IQNA

Gazeti la Guardian

Waislamu Uingereza wapuuza mpango wa vita dhidi ya ugaidi

19:57 - December 26, 2015
Habari ID: 3469676
Waislamu nchini Uingereza wamepuza mpango wa serikali ya nchi hiyo wa kupambana na ugaidi na wametangaza kuususia.

Takwimu rasmi za serikali ya Uingereza imesema kuwa kumeshuhudiwa kupungua kwa kiasi kikubwa ushirikiano wa Waislamu aktika mpango maalumu wa kupambana na ugaidi uliopewa jina la Prevent. Taarifa zinasema sababu ya hilo ni kuwa Waislamu hawajaridhishwa na mpango huo na wala hawaiamini serikali ya Uingereza.
Kwa mujibu wa gazeti la Guardian, jamii za Waislamu zimetoa asilimia 10 tu ya taarifa zilizopokewa katika mpango huo wa kistratijia wa kupambana na ugaidi.
Hii ni katika hali ambayo, afisa mmoja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza amesema baadhi ya misikiti na taasisi za kidini zina jukumu la kutoa taarifa kwa serikali kuhusu yeyote anayeshukiwa kuwa gaidi au mwenye misimamo ya kigaidi. Mapema mwaka huu pia Pilisi ya Uingereza ilitangaza kuwa kati ya taarifa 3288 zilizotolewa katika mapngo huo wa vita dhidi ya ugaidi, asilimia 8 tu ndio zilizotoewa na Waislamu.

3469641

captcha