IQNA

Ireland yasema ni sharti mawakili kuwa na Qur'ani kwa ajili ya kiapo

11:32 - April 25, 2016
Habari ID: 3470270
Jumuiya ya Mawakili nchini Ireland, imewashurutisha mawakili wanaowahudumia Waislamu kutumia Qur'ani Tukufu wakati wa kula kiapo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, gazeti la Sunday Independent limeripoti kuwa, Peter Kelly, Jaji wa Mahakama Kuu ya Ireland ametoa amri ya kuwawajibisha mawakili nchini humo kuapa kwa kutumia vitabu vyao vitakatifu.

Kabla ya hapo jamii ya wanasheria wa Ireland ilikuwa imewataka kwa siri wanachama wake wahakikishe kuwa watumie vitabu vitakatifu kutekeleza viapo vya watu wanaowawkilisha.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, Wakristo na Mayahudi nao wanatakiwa kula viapo kwa kutumia vitabu vyao.

Takwimu zinaonesha kuwa, hadi mwaka 2013, Ireland ilikuwa na karibu watu milioni nne na nusu huku idadi ya Waislamu ikiwa ni zaidi ya elfu hamsini.

3491463

captcha