IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Waislamu wakabiliane na magaidi wakufurishaji pamoja vibaraka wa Marekani, Israel

22:55 - May 20, 2016
Habari ID: 3470322
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran ametoa wito kwa Waislamu kukabiliana na magaidi wakufurishaji pamoja na serikali vibaraka ambazo zinapata uungaji mkono wa Marekani na Utawala wa Kizayuni katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Ayatullah Mohammad Imami Kashani katika hotuba zake za Sala ya Ijumaa hii leo ameashiria nafasi ya madola ya kibeberu na kiistikbari katika kupora utajiri wa Mashariki ya Kati sambamba na kuvunja nguvu za Uislamu na kusema: "Umoja wa Waislamu na mwamko wao mbele ya maadui wa Uislamu ni jambo litakalo vunja njama zao."

Aidha amesema Marekani na waitifaki wake kamwe hawataki kuona ustawi na maendeleo ya nchi za Kiislamu na wanafanya kila wawezalo hata mauaji na ukatili ili kuvuruga usalama wa eneo.

Ayatullah Imami Kashani ameashiria sisitizo na tahadhari alizotoa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu njama za madola ya kibeberu katika kueneza chuki dhidi ya Uislamu na Iran na kusema kuwa: "Mauaji na jinai zinazotendeka leo kwa jina la Uislamu huko Iraq, Yemen na Syria ni katika fremu ya chuki dhidi ya Uislamu na Iran."

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amekosoa baadhi ya nchi za eneo ambazo zinafuata sera za Marekani na Utawala wa Kizayuni wa Israel kukiuka maslahi ya mataifa ya eneo kwa kuunga mkono makundi kigaidi na wakufurishaji na kueleza kwamba: "Kukabiliana na njama hizi kunahitaji mwamko wa Kiislamu na umoja katika umma wa Kiislamu".

Aidha amesema taifa la Iran liko macho kabisa kuhusu njama za Marekani katika eneo. Ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina usalama na mshikamano kutokana na uongozi wa busara wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Aidha amepongeza hatua ya bunge la Iran kupitisha muswada wa sheria ambayo itailazimu Marekani iilipe Iran fidia kutokana na jinai zake dhidi ya Iran na Wairani.

3499719

captcha