IQNA

OIC yazitaka nchi Kiislamu kuwakumbuka na kuwasaidia mayatima

19:03 - June 14, 2016
Habari ID: 3470387
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imetoa wito kwa nchi za Kiislamu duniani na mashirika ya kutoa misaada kuwasaidia mayatima hasa kwa mnasaba wa Siku ya Mayatima Katika Nchi za Kiislamu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, OIC imetoa taarifa na kusema, maafa, vita na migogoro katika nchi nyingi za Kiislamu ni jambo ambalo limepelekea kuwepo mamia ya maelfu ya watoto yatima.

Taarifa hiyo imesema Uislamu, zaidi ya dini zingine zote, umesisitiza sana suala la kuwapa haki na kuwasaidia mayatima. OIC imetaka suala la mayatima kote duniani lipewe umuhimu na uzito unaostahiki.

NI kwa msingio ndio OIC ikaamua kutenga tarehe 15 ya Mwezi Mtukufu wa Ramahdani kuwa 'Siku ya Mayatima Katika Ulimwengu wa Kiislamu' ili kwa njia hiyo kuwakumbusha Waislamu kuhusu jukumu lao la kuwasaidia mayatima kila wakati. OIC inawakumbusha Waislamu wenye uwezo duniani kuhusu haja ya kuwakirimi mayatima na kuwaondolea masiabu sambamba na kuwalinda.

Ikumbukwe kuwa katika Kikao cha 40 cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa OIC kilichofanyika Guinea Conakry, Desemaba 9-11 mwaka 2013, iliamuliwa kuwa tarehe 15 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kila mwaka iwe 'Siku ya Mayatima Katika Ulimwengu wa Kiislamu' ili kwa njia hiyo kuwakumbusha Waislamu kuhusu mayatima na mahitajio yao.

3460080

Kishikizo: oic kiislamu mayatima iqna
captcha