IQNA

Wairani 85,000 kushiriki katika ibada ya Hija mwaka huu

11:55 - March 18, 2017
Habari ID: 3470899
TEHRAN (IQNA)-Wairani zaidi ya 85,000 wanatazamiwa kushiriki katika ibada ya Hija mwaka huu kufuatia mapatano baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Shirika la Hija na Ziara ya Iran Ijumaa limetangaza kuwa, , Iran imeafiki wananchi wake wende kuhiji baada ya utawala wa Saudi Arabia kuahidi kutekeleza matakwa ya Iran na kutokana na sisitizo la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, viongozi wa serikali na wananchi kuhusu utekelezaji wa ibada ya Hija yenye hadhi na kwa kuzingatiwa misingi ya amani, izza na utukufu wa mahujaji wa Kiirani na vilevil kudhaminiwa huduma zinazohusiana na viza, tiba na kadhalika.

Taarifa hiyo imesema kuwa, taarifa kamili kuhusu mazungumzo ya masuala mbalimbali likiwemo suala la mashahidi waliopoteza maisha katika eneo la Mina na Msikiti Mtakatifu wa Makka katika ibada ya Hija ya mwaka juzi itatolewa baadaye.

Awali mkuu wa Shirika la Hija na Ziara ya Iran, Hamiid Muhammadi alikuwa amesema kuwa miongoni mwa masharti ya kuanza tena safari za Hija kwa Waislamu wa Iran ni kudhaminiwa haki zinazohusiana na masuala ya viza za mahujaji wa Kiirani, udharura wa serikali ya Saudi Arabia kutoa dia ya mahujaji 464 walioaga dunia katika eneo la Mina kwenye ibada ya hija ya mwaka juzi, kulindwa heshima na utukufu wa mahujaji na vilevile kudhaminiwa usalama na utulivu wakati wa ibada ya Huja.

Mnamo Septemba 2015, kulijiri msongamano mkubwa wakati wa ibada ya Hija katika eneo la Mina karibu na Makka ambapo duru zisizo rasmi zinasema Mahujaji 7,000 walipoteza maisha huku Saudia ikisisitiza ni watu 770 waliouawa katika msongamano huo. Iran ilitangaza kuwa mahujaji wake wapatao 465 walipoteza maisha katika maafa hayo ya Mina. Siku kadhaa kabla ya tukio hilo, Mahujaji 100 walipoteza maisha katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, wakiwemo Wairani 11 baada ya winchi kuwaangukia wakati wanapotufu.

Maswali mwengi waliibuka kuhusu uwezo wa Saudi Arabia kusimamia zoezi la Hija ambapo mwaka jana Iran ilitaka usalama wa Mahujaji wake udhaminiwe. Kufuatia sisitizo hilo la Iran, Saudi Arabia mwaka jana iliwazuia mahujaji Wairani kushiriki katika ibada ya Hija.

3584897/

captcha