IQNA

Iran kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Umma nchini Kenya

11:47 - July 23, 2018
Habari ID: 3471604
TEHRAN (IQNA) Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itashirikiana na Chuo Kikuu cha Umma nchini Kenya ambacho ni chuo kikuu cha kwanza cha Kiislamu katika nchi hiyo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, hayo yamebainika hivi karibuni katika mkutano baina ya Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Kenya Bw. Mahmoud Majlisein na Dr. Idle Farah Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Umma. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za chuo hicho katika Kaunti ya Kajiado nje kidogo ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Mazungumzo hayo yalihusu ushirikiano katika kuandaa makongamano na pia nyuga mbali mbali za uhusiano na vyuo vikuu vya Iran. Aidha walijadili kuhusu mafunzo ya taaluma ya Iran au Iranology katika Chuo Kikuu cha Umma na kupewa nafasi wanafunzi wa chuo hucho kujiendeleza kimasomo nchini Iran.

Bw. Majlisein amesema tayari ofisi yake inashirikiana na vyuo vikuu nchini Kenya kama Chuo Kikuu cha Kenyatta ambapo kuna mpango wa kuanzisha mafunzo ya lugha ya Kifarsi katika chuo hicho.

Chuo Kikuu cha Kiislamu nchini Kenya ilianzishwa mwaka 2013 na hivi sasa kina idara kadhaa za masom zikiwemo idara ya sayansi ya kompyuta, idara ya biashara, idara ya masomo ya Kiislamu, idara ya sharia za Kiislamu na idara ya masomo ya uuguzi.

3731933

captcha