IQNA

Muiraqi ashinda mashindano makubwa zaidi duniani ya Qur'ani mubashara kupitia televisheni

9:15 - June 07, 2019
Habari ID: 3471989
TEHRAN (IQNA) – Qarii (msomaji wa Qur'ani) kutoka Iraq ameibuka mshindi katika Duru ya 12 ya mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur'ani (qiraa) ambayo hufanyika mubashara au moja kwa moja kupitia Televisheni ya Al Kauthar ya Iran.

Kwa mujibu wa Idara ya Mawasiliano ya Umma katika Kanali ya Televisheni ya Al Kauthar, Muiraqi Falah Zulayf ameibuka mshhindi kwa kupata pointi 92.25 na Tajweed bora zaidi. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Ahmed al Sayyed al Ahmad al Sayyed al Ghaytani wa Misri ambaye alipata pia pointi 92.25. Waliofuata kwa taratibu ni Mohammad Mohammadi wa Ujerumani, Seyed Foad Shokavi wa Iran na Mohsen Shojaei wa Afghanistan .

Mashindano hayo yaliyopewa anuani ya إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا , "Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu" hufanyika kila mwaka kwa njia ya simu na kuanza katika usiku kwa kwanza wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Mwaka huu  mashindano hayo yalikuwa na washiriki 200 ambapo 96 waliingia nusu fainali na hatimaye watano miongoni mwao wakaingia fainali.

Fainali zilifanyika katika usiku wa kuamkia Idul Fitr. Kwa mujibu wa Sayyed Razavi, jopo la majaji wanaojumuisha wataalamu wa Qur'ani Tukufu kutoka Iran na nchi kadhaa wanatazamiwa kusimamia mashindano hayo ya Qur'ani.

Televisheni ya Al Kauthar ni katika televisheni zinazosimamiwa na Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

3817338

captcha