IQNA

Wazazi Waislamu Uingereza wataka watoto wapewe chanjo halali

10:40 - July 30, 2019
Habari ID: 3472063
TEHRAN (IQNA) - Wazazi Waislamu nchini Uingereza wamekataa watoto wao wapewe chanjo ya homa baada ya Baraza la Wauslamu Uingereza kubaini kuwa chanjo hiyo si halali.

Maafisa wa afya nchini humo wamebainisha wasiwasi wao kutokana na idadi kubwa ya watoto Waislamu ambao watasusia mpango wa chanjo ya homa utakaoanza mwezi ujao.
Wazazi Waislamu wamesema chanjo hiyo ambayo ni maarufu kama Fulenz Spray ni haramu kwa sababu ina gelatin iliyotokana na nguruwe ambayo imeharamishwa katika Uislamu.
"Tumeshauriana na wanazuoni kuhusu suala hili na mtazamo wao ni kuwa tunahitaji chanjo ambayo ni halali," amesema Daktari Shuja Shafi, mwenyekiti wa Kamati ya Utafiti katika Baraza la Waislamu Uingereza.

Kufuatia hali hiyo chuo cha afya cha Royal College of Public Health kimetahadharisha kuhusu hatari ya mripuko mkubwa wa homa Uingereza na kutoa wito kwa serikali kutoa chanjo halali.

3469072

captcha