IQNA

Mwanaanga wa UAE kupeleka nakala ya Qur'ani anga za mbali

14:45 - August 28, 2019
Habari ID: 3472104
TEHRAN (IQNA) – Mwanaanga wa kwanza wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kufika katika anga za mbali amesema atabeba nakala ya Qur'ani katika safari yake hiyo ya kihistoria.

Hazza Al Mansouri atakuwa mwanaanga (astronaut) wa kwanza wa UAE na hivi sasa anajitayarisha kuelekea katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Mbali (ISS) Septemba 25.

Al Mansour amesema atabebe nakala ya Qur'ani katika safari hiyo ambapo atatumia chombo cha kusafiri katika anga za mbali kinachojulikana kama Soyuz MS 15 na atakaa katika kituo hicho cha ISS kwa muda wa siku nane kabla ya kurejea katika sayari ya dunia.

Katika safari hiyo ataandamana na wanaanga Oleg Skripochka wa Russia na Jessika Meir wa Marekani. Wakiwa katika kituo cha ISS watafanya majaribio kadhaa ya kisayansi kabla ya kurejea katika sayari ya dunia Oktoba 3.

Akiwa katika anga za mbali, Al Mansouri pia atatayarishiwa chakula halali.

3837974

captcha