iqna

IQNA

Kutuhusu

Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

 

Kutuhusu

Lijue Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA)

 

Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) ndio la kwanza na la pekee ambalo linashughulikia kwa njia maalumu habari za Quran katika ulimwengu wa Kiislamu. Shirika hili lilianzishwa Novemba 11, 2003 sambamba na tarehe 11 ya Mwezi Aban (Kalenda ya Hijria Shamsia) sawa na tarehe 15 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka 1424 Hijria Qamaria katika sherehe iliyohudhuriwa na rais wa wakati huo wa Iran.

 

Shirika hili lilianza kwa habari 7 kwa siku kwa lugha ya Kifarsi na baada ya kupita miaka 19 ya kazi, shirika hili sasa, kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu, linazalisha takribani habari 850 kwa siku kwa lugha 21 duniani ambapo hadi sasa habari zinazohusiana na Qur'ani zilizoandikwa zimepindukia milioni moja na laki tatu.

Kwa kuzingatia anuai ya lugha na ujumbe wa kimataifa wa IQNA, shirika hili mwezi Machi mwaka 2013 lilipata kibali cha Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran na kubadilisha jina kutoka Shirika la Habari la Qur’ani la Iran na kuwa Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) ili kwa njia hiyo, sawa na Qur'ani Tukufu, liweze kuwa kiunganishi cha Waislamu kote duniani.


Malengo:

Malengo muhimu yanayozingatiwa na Shirika la Habari la Qur'ani la Iran IQNA ni kama ifuatavyo:

· Kupasha haraka habari kamili kuhusu harakati na shughuli zinazohusiana na Qur’ani Tukufu nchini Iran na duniani kote.

· Kuakisi mazingira ya Qur'ani Tukufu yanayotawala katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi nyinginezo za Kiislamu duniani.

· Kuhimiza jamii ilelekee katika mtindo wa maisha kwa msingi wa Qur’an Tukufu

· Kujitahidi kuhakikisha kuwa mafundisho ya Qur’ani Tukufu yanatumika kama mhimili mkuu katika sekta mbali mbali

· Kuwabainishia Waislamu duniani kuhusu harakati za Qur'ani katika mfumo mtakatifu wa Jamhuri ya Kiislamu

 

Lugha za IQNA:

Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA)hivi sasa linatayarisha habari za Qur'ani kwa lugha 21 hai za dunia zikiwemo: Kifarsi, Kiarabu, Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Kiurdu, Kitaliano, Kichina, Kirussia, Kihispania, Kibengali, Kihausa, Kipashtu, Kihindi, Kituruki, Kiazari na Kimalayu, Kiindonesia, Kifilipino, Kijerumani na Kireno.

 

Matawi ya IQNA:

Ili kufanikiwa IQNA katika katika kila kona ya dunia, shirika hili la habari za Qur'ani limeanzisha matawi mikoani nchini Iran na katika nchi za kigeni. Hivi sasa kuna matawi ya IQNA katika mikoa 30 ya Iran na pia katika nchi sita duniani ifuatavyo.

1. Matawi ya IQNA mikoani ni kama ifuatayo:

Ilam, Azerbaijan Magharibi, Azerbaijan Mashariki, Ardabil, Alborz, Isfahan, Bushehr, Sistan na Baluchistan, Chehar Mahal na Bakhtiari, Khuzestan, Khorassan Razawi, Khorassan Kaskazini, Kermanshah, Gilan, Fars, Mazandaran, Markazi, Hormozgan, Hamedan na Yazd.

 

2.Maeneo ya kigeni

Eneo la Magharibi mwa Asia

Eneo la Mashariki mwa Asia

Eneo la Asia ya Kati

Eneo la Ulaya

Eneo la Afrika

Eneo la Amerika

 

Huduma za Habari:

Kutokana na kuwa lengo la IQNA ni kueneza utamaduni wa Qur'ani katika nyanja mbali mbali za kidini, kisiasa, kisanaa, kijamii, kiuchumi nk, katika kuanzisha idara na vitengo vyake vya habari, IQNA imezingatia mahitajio ya wasomaji na udharura uliopo katika kubainisha ufahamu wa Qur'ani Tukufu. IQNA inazingatia yafuatayo katika kuanzisha vitengo idara zake kuu: A. Matuko: Hapa matukio yanajumuisha kupasha habari kuhusu yaliyojiri katika setka au nyanja mbali mbali na B.Maudhui. Idara hiihufuatilia maudhui mbali mbali za Qur'ani kwa kuzingatia mahitaji ya wasomaji wa kila eneo na sera jumla za IQNA. Maudhui za Qur'ani katika IQNA hutegemea ushauri wa wasomi na wataalamu ambao hufanyiwa mahojiano na kisha waliyoyasema kuchapishwa katika jarida maalumu la kidijitali.

IQNA hivi sasa ina vitengo 8 asili na vitengo vingine 64 vidogo vya habari ifuatavyo.

1. Harakati za Qur'ani (Harakati za Qur'ani, taasisi za Qur'ani za wananchi, shakhsia na waandishi habari wa kujitolea).

2. Siasa na Uchumi (Siasa na Uchumi)

3. Maarifa ya kidini ( Hapa wahusika ni wasomi na wanafikra wa vyuo vya kidini au Hawza na vyuo vikuu)

4. Kijamii (jamii, afya na mitandao ya intaneti)

5. Sanaa na Fasihi (sanaa, fasihi, jihadi na hamasa)

6. Kimataifa (Kifarsi, Kiarabu, Kiingereza, Kiswahili, Kirussi na lugha nyinginezo)

7. Mikoa

8. Media anuai na picha.

Kitengo cha waandishi habari wa kujitolea wa IQNA, kilianzishwa mwaka 2003 kwa lengo la kuwa na waandishi habari ambao wanajitolea kukidhi mahitaji ya kila siku ya habari za Qur'ani kote nchini Iran. Kundi hili hivi sasa lina waandishi habari 7,268 waliojiandikisha ambapo 5,300 kati yao hutuma habari mara kwa mara. Kwa wastani kitengo hiki hupokea habari 120.

Shirika la Habari za Qura'ni la Kimataifa (IQNA) mbali na mipango na malengo hayo yaliyoainishwa pia linafuatilia na kutekeleza mipango ifuatayo.

· Kuandaa vikao vya kitaalamu

· Kuchapisha jarida la "Rayhe” (Harufu Nzuri)

· Kuandaa na kushiriki katika makongamano ya Qur'ani Tukufu