IQNA

Kitabu cha “Qur’ani Nchini Russia” chachapishwa

10:51 - December 23, 2008
Habari ID: 1721861
Kitabu cha “Qur’ani Nchini Russia” kilichoandikwa na Arif Aliov kimechapishwa mjini Moscow kwa lugha ya Kirussia.
Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Iran mjini Moscow Abu Dharr Ibrahimi Turkman amesema kuwa taasisi ya “Urafiki wa Mataifa” ndiyo iliyochapisha kitabu hicho chenye kurasa 384. Amesema kuwa mwandishi wa kitabu hicho Arif Aliov ni mtaalamu wa masuala ya Kiislamu na ana shahada ya udaktari wa historia kutoka Chuo Kikuu ch Saint Petersburg nchini Russia.
Ibrahimi amesema: Kitabu hicho kimechapishwa kwa lugha ya Kirussia ili kuwasaidia wazungumzaji wa lugha hiyo kuelewa vyema aya za Qur’ani na athari za mafundisho ya aya hizo katika maisha ya mwanadamu iwapo zitafanyiwa kazi.
Ibrahimi ameongeza kuwa, sehemu kubwa ya kitabu hicho inajibu madai yaliyokuwa yakitolewa katika kipindi cha serikali ya Muungano wa Sovieti kwamba Uislamu ni dini inayowaunga mkono mabepari na kuwadhalilisha wanawake na thamani za kibinadamu.
Katika sehemu nyingine ya kitabu hicho mwandishi amejadili maudhui ya hali ya wananchi wa bara Arabu kabla ya kudhihiri Uislamu, Uislamu ulivyodhihiri, kubaathiwa kwa Mtume Muhammad (saw) na jinsi dini ya Kiislamu ilivyoenea katika zama za Mtume na baada ya kufariki kwake dunia. 337026
captcha