Kongamano hilo linasimamiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Sayansi na Utamaduni ya Sweden kwa lengo la kumuarifisha Mtume wa Uislamu kwa raia wa nchi hiyo.
Ajenda ya kongamano hilo ni pamoja na mihadhara itakayozungumzia sifa na shakhsia ya Mtume Muhammad (saw), ugavi wa vitabu vinavyojadili sira na maisha ya mtukufu huyo na maonyesho ya vitabu na maandiko ya wataalamu wa masuala ya Mashariki kuhusu Nabii wa Uislamu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kimataifa ya Sayansi na Utamaduni ya Sweden amesema kuwa jumuiya hiyo imeshirikiana na wahubiri wa Kiislamu na wanafunzi wa vyuo vikuu kutayarisha zaidi ya vitabu elfu kumi kwa lugha ya Sweden na lugha nyingine hai duniani kama Kiingereza, Kifaransa, kihispania, Kijerumani, Kiholanzi, Kinorway na Kirussia ambavyo vinazungumzia maisha ya Nabii Muhammad (saw). 429611