Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Yusuf Saeed, Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kiislamu cha Imarati amesema watu hao waliosilimu walikuwa wamekwenda Imarati kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kibiashara na kitalii. Amesema watu hao wamevutiwa na Uislamu na baada ya kutafuta muongozo katika idara za kutoa maelezo kuhusu Uislamu, walikubali kusilimu.
Ameongeza kuwa vituo vya Kiislamu vya Imarati vijulikanavyo kama Darul Birr ndivyo ambavyo hutoa maelezo kuhusu Uislamu kwa kutumia mbinu za hekima. Amesema vituo hivyo vimefasiri vitabu vya Kiislamu na Qur'ani Tukufu kwa lugha za Kiingereza, Kichina, Kirussia, Kifaransa , Kiurdu na lugha nyiginezo zinazotumiwa na wanaosilimu. Ameongeza kuwa vitabu hivyo hutolewa kwa wanaohitajia na kwamba katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, vituo hivyo vimesambaza vitabu elfu kumi katika maeneo mbalimbali ya Umoja wa Falme za Kiarabu.
627741