IQNA

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu asisitiza kushikamana na matukufu ya Kiislamu

8:26 - August 31, 2010
Habari ID: 1984849
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kushikamana na matukufu ya Kiislamu na ya Jamhuri ya Kiislamu, kupigania uadilifu na kupambana na ubeberu ni mambo muhimu sana.
Ayatullahil Udhma Khamenei alisema hayo jana alipoonana na Rais na Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hapa mjini Tehran kwa mnasaba wa Wiki ya Serikali na katika kukumbuka siku walipouawa shahidi Rais na Waziri Mkuu wa zamani wa Iran yaani shahidi Rajai na shahidi Bahonar na kuongeza kuwa, mashahidi hao watukufu ni dhihirisho la uchapaji kazi, imani na kushikamana vilivyo na misingi na matukufu ya Jamhuri ya Kiislamu.
Ayatullahil Udhma Khamenei vile vile ameelezea kufurahishwa kwake na kitendo cha serikali ya Iran cha kulipa umuhimu maalumu suala la utamaduni na kazi za kidiplomasia na kuongeza kuwa, pamoja na kuwa kazi za serikali na harakati zake za kidiplomasia ni nzuri, lakini kitu kilicho muhimu zaidi kuliko harakati za kisiasa na kidiplomasia ni roho na mikakati iliyomo ndani kazi hizo za kidiplomasia na harakati za kisiasa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesema, Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ina jukumu la kuongoza na kusimamia masuala yote ambayo kwa namna fulani yanahusiana na siasa za nje na uhusiano wa Iran na mataifa mengine kwa umakini wa hali ya juu.
645357
captcha