Amesema Iran inataka ustawi wa elimu kwa ajili ya kupata uwezo halisi na kupeperusha bendera ya uadilifu na ubinadamu kote duniani ili pamoja na kuwatetea wanaodhulumiwa, tuweze kusimama kidete mbele ya dhulma na uonevu wa madhalimu na wanaopenda ukubwa na jaha.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa sisitizo la Jamhuri ya Kiislamu juu ya udharura wa maendeleo ya elimu na sayansi ni jambo linalofanyika kwa mahesabu maalumu kwani mahesabu yakinifu yanaonyesha kwamba elimu na sayansi ndio msingi wa nguvu na maendeleo ya kimaada na kiroho ya nchi yoyote ile na taifa linalobakia nyuma katika uwanja huo hulazimika kuyafuata mataifa mengine.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa lengo la maendeleo ya kisayansi katika mfumo wa Kiislamu linatofautiana na malengo ya nchi za Magharibi. Ameashiria maafa yaliyosababishwa na nchi za Magharibi katika maeneo mbalimbali duniani kwa kutumia maendeleo yao ya kisayansi na akasema: “Lengo la nchi za Magharibi katika medani ya maendeleo ya kisayansi lilikuwa ni kupata utajiri na kwa msingi huo nchi hizo hazikujali wala kuheshimu maadili, imani na haki za watu katika kuamiliana na mataifa ya bara Hindi, Afrika, mashariki mwa Asia na America ya Latini.”
Amesema kuwa kushadidi dhulma, ufa baina ya matabaka mbalimbali na kupuuzwa kwa haki za kimsingi za mataifa mbalimbali ni miongoni mwa matokeo ya malengo yasiyokuwa sahihi ya elimu na sayansi katika nchi za Magharibi. Ameongeza kuwa katika Uislamu suala la kutakasa nafsi limetangulizwa mbele ya kutafuta elimu kwani iwapo hakutakuwepo utakasaji na malezi ya nafsi ya mwanadamu elimu na sayansi itakuwa wenzo wa uhabithi na kutenda jinai na uhalifu.
Amesema kuwa lengo la juhudi kubwa za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika njia ya ustawi na maendeleo ya sayansi na teknolojia ni kustawisha matukufu ya kibinadamu na kutetea haki za mwanadamu. Amesema Iran inataka ustawi wa elimu kwa ajili ya kupata uwezo halisi na kupeperusha bendera ya uadilifu na ubinadamu kote duniani ili pamoja na kuwatetea wanaodhulumiwa, tuweze kusimama kidete mbele ya dhulma na uonevu wa madhalimu na wanaopenda ukubwa na jaha.
Mwishoni mwa hotuba yake, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa wasomi bingwa, wanafunzi wa vyuo vikuu, wahadhiri, viongozi na wananchi wote wa Iran watafungua njia mpya katika medani ya malengo ya ustawi na maendeleo ya kisayansi na kupeperusha bendera ya thamani za Kiislamu kote duniani baada ya kupata uwezo wa kielimu ambao ndio nguzo ya nguvu ya kimaada na kimaanawi. 669906