IQNA

Fatuwa ya Kiongozi Muadhamu, hatua muhimu ya kukurubisha pamoja madhehebu ya Kiislamu

23:04 - October 10, 2010
Habari ID: 2010183
Msemaji wa Chuo Kikuu cha al Azhar cha Misri amepongeza fatuwa iliyotolewa hivi karibuni na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Ayatullah Ali Khamenei akiharamisha hatua yoyote ya kuvunjia heshima shakhsia wa Kiislamu wanaoheshimiwa na Ahlusunna na kusema kuwa hiyo ni hatua muhimu katika njia ya kukurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu na kuzima njama za maadui za kutaka kuzusha fitina na mifarakano.
Muhammad Rafa’ al Tahawi amesema kuwa fatuwa hiyo ya Ayatullah Khamenei imetolea wakati mwafaka na mmoja wa maulama wakubwa wa Kishia.
Ameongeza kuwa fatuwa hiyo ina sehemu mbili muhimu ambazo ni upande wa kisiasa na kukurubisha pamoja Waislamu na harakati ya kuondoa sababu za hitilafu na mifarakano kati ya wafuasi wa madhehebu mbalimbali za Kiislamu.
al Tahawi amesema sehemu ya pili ya fatuwa hiyo ni kueleza misimamo ya wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbait na Shia kuhusu masahaba wa Mtume (saw).
Mtafiti huyo wa masuala ya kukurubisha pamoja Waislamu wa Misri amesisitiza kuwa fatuwa hiyo imetolewa na mmoja kati ya wanazuoni wakubwa wa Kishia na itakuwa na taathira kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu.
Msemaji wa Chuo Kikuu cha al Azhar amesema kuwa Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni wanapaswa kusisitiza juu ya masuala yanayowakutanisha pamoja na kuwa macho na njama za maadui za kutaka kuwatenganisha. 670999

captcha