IQNA

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu:

Imani kwa Mwenyezi Mungu na kujitolea katika njia yake ndiyo siri ya nguvu ya Iran

12:48 - October 21, 2010
Habari ID: 2017006
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amehutubia umati mkubwa wa familia za mashahidi na walemavu wa vita wa mkoa wa Qum akisema kuwa itikadi ya kufa shahidi na imani juu ya suala la kujitoa mhanga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ndio siri ya fahari halisi ya taifa la Iran.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amehutubia umati mkubwa wa familia za mashahidi na walemavu wa vita wa mkoa wa Qum akisema kuwa itikadi ya kufa shahidi na imani juu ya suala la kujitoa mhanga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ndio siri ya fahari halisi ya taifa la Iran. Amesisitiza kuwa taifa hili litaendelea kusimama kidete mbele ya tamaa za mabeberu chini ya kivuli cha masuala hayo yaliyolipa fahari na utukufu.
Katika hadhara hiyo iliyogubikwa na anga ya masuala ya kiroho na kimaanawi ya kuwakumbuka mashahidi watukufu, Ayatullah Khamenei amekutaja kuuawa shahidi kuwa ni maudhui kubwa mno na kuongoza kwamba kuwa na itikadi ya kufa shahidi na kuamini kwamba mashahidi wana adhama na utukufu mkubwa ndio sura ya kimaanawi na kiroho ya utambulisho wa taifa.
Amesema kuwa imani, hisia za kidini, ushujaa wa wananchi na subira na ukakamavu wa familia za mashahidi umepelekea kutatuliwa suala la kuuawa shahidi kwa wananchi wa Iran. Amesema kuwa katika nukta hii muhimu inatupasa kutafakari na kujiuliza kwamba ni vipi na kwa njia gani taifa la Iran limeweza kuwa na fahari, utukufu, mvuto na uwezo mkubwa kama huu katika macho ya mataifa mbalimbali na kuwa na taathira katika matukio mbalimbali ya dunia bila ya kuwa na nyenzo tata za kijeshi na suhula kubwa za kipropaganda?
Ayatullah Khamenei amesema kuwa mapokezi makubwa ya wananchi wa Lebanon kwa Rais Mahmoud Ahmadinejad wa taifa la Iran ni maudhui inayostahili kufanyiwa uchunguzi na uchambuzi. Ameongeza kuwa ukweli huo unadhihirisha mvuto na adhama ya taifa la Iran kwa mataifa mengine.
Akifafanua sababu za adhama na mvuto huo, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia umuhimu wa daraja ya kuuawa shahidi na kusema kuwa: "Wakati taifa lolote na vijana wake linapokuwa na imani kubwa ya kujitolea, kujitoa mhanga na kuuawa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, hapana shaka kwamba litapata uwezo, utukufu na adhama iliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu; ni kwa sababu hiyo ndiyo maana hii leo taifa la Iran limekuwa na nguvu na adhama kubwa zaidi ya mataifa mengine."
Akiashiria taathira isiyokuwa na kifani ya mashahidi katika adhama na utukufu wa taifa la Iran, Ayatullah Khamenei amesema kuwa mashahidi, vilema wa vita na kadhalika ndio vinara na wabeba bendera ya kambi ya haki na wamewafunza kivitendo watu wa nchi hii itikadi ya kuuawa shahidi na jinsi ya kujitolea mhanga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Ameongeza kuwa katika safu ya pili ya sababu za adhama ya taifa la Iran kuna baba wenye subira, mama wenye nyoyo zilizopatwa na msiba, watoto waelewa na wake azizi wa mashahidi ambao walihisi fahari mkabala wa tukio linaloonekana kidhahiri kuwa chungu la kuachwa mkono na vipenzi vyao na kuonyesha kuwa kama walivyokuwa mashahidi wapenzi, wao pia wana imani ya kufanya muamala na Mwenyezi Mungu na wako katika njia halisi ya Bibi Zainab bint Ali bin Abi Twallib (as).
Ayatullah Khamenei amesema kuwa kusimama kidete taifa la Iran na familia za mashahidi mbele ya vitisho vya mabeberu wa kimataifa kunatokana na hisia ya kuwa na nguvu na kujiamini kitaifa. Amesema kuwa taifa la Iran kamwe halitalegeza msimamo na thamani zake kutokana na vitisho vya madhalimu.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza juu ya udharura wa kuimarishwa imani kwa Mwenyezi Mungu katika nyoyo za wananchi na viongozi na akasema kuwa tunapaswa kutambua thamani ya imani hii na kuifanya nguzo ya maendeleo ya kisayansi, kiteknolojia, kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Ayatullah Ali Khamenei amezungumzia pia njama na mipango mingi iliyotekelezwa na maadui na vibaraka wao hapa nchini katika miaka ya baada ya kuaga dunia hayati Imam Khomeini kwa shabaha ya kudhoofisha imani na itikadi za taifa na kusema kuwa maadui wa taifa la Iran hawakuambulia lolote kutokana na njama hizo ghairi ya kushindwa na hali ya mambo itaendelea kuwa hivyo.
Amewasifia vijana wa Iran na akasema kuwa kizazi hiki cha vijana kilichokulia katika anga ya imani na itikadi za taifa ni kizazi chenye baraka nyingi na kiko tayari kujitolea na kujitoa mhanga kama kilivyokuwa kizazi cha mwanzoni mwa Mapinduzi ya Kiislamu.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa mji wa Qum uliotoa mashahidi elfu sita, vilema wa vita elfu 11 na nyota mashuhuri za mashahidi kama Zainuddin, Haidariyan na Sadiqi, umekuwa mstari wa mbele pia katika suala la mashahidi.
Mwanzoni mwa mkutano huo Hujjatul Islam Wakili ambaye ni baba wa mashahidi watatu na kilema mmoja wa vita, alimkaribisha Kiongozi Muadhamu katika mji wa Qum.
Mama wa mashahidi mawili Mahdi Zainuddin, aliyekuwa kamanda wa kikosi cha 17 cha Ali bin Abi Twalib, na Majid Zainuddin amesisitiza kuwa wamefunga mkataba na mashahidi wa kuwa waaminifu kwa utawala wa faqihi na thamani nyingine za Kiislamu na kimapinduzi kama walivyokuwa wao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri na mkuu wa Taasisi ya Mashahidi ya Iran Muhandisi Zaribafan pia amehutubia hadhara hiyo akiashiria mashahidi elfu 6 na vilema elfu 11600 wa vita wa mkoa wa Qum na akasema kuwa wananchi wa mkoa huo wamekuwa mstari wa mbele katika kutetea Uislamu na uongozi wa juu wa dini katika vipindi nyeti vya kabla na baada ya Mapinduzi ya Kiislamu na vilevile katika kipindi cha vita vya kujitetea kutakatifu. 679324
captcha