Ayatullah Khamenei ameyasema hayo Jumatatu Desemba 6 katika mkutano wake na maafisa wa msafara wa hija wa Iran.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa viongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ni wabeba bendera ya umoja katika ulimwengu wa Kiislamu.
Ameashiria umuhimu wa kuwepo umoja wa Kiislamu na kusisitiza udharura wa kupunguzwa hitilafu kati ya Waislamu wa Shia na Suni. Amesema kuwa viongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu walikuwa vinara na wabeba bendera ya umoja na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu hata kabla ya ushindi wa mapinduzi hayo.
Ayatullah Khamenei amewashukuru maafisa wa msafara wa hija wa Iran kwa kuendesha vizuri kazi hiyo na akasema kuwa licha ya kazi nzuri zilizofanyika lakini hatupasi kufumbia macho nakisi na kasoro zilizokuwepo. Ametilia mkazo suala la kupunguzwa kasoro hizo hadi kufikia kiwango cha kuridhisha.
Ayatullah Khamenei amesema watu wanaokwenda hija wanapatwa na mabadiliko makubwa kwa kushuhudia usafi, masuala ya kiroho na adhama ya maeneo matukufu ya Makka na Madina, lakini jambo muhimu zaidi ni kulinda matunda hayo ya kiroho.
707875