IQNA

Wabunge Masuni Iran walaani hujuma ya kigaidi Chabahar

14:31 - December 20, 2010
Habari ID: 2050331
Wabunge Masuni katika Bunge (Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu) ya Iran wamelaani hujuma ya kigaidi ya wiki iliyopita katika siku ya Tasu'a katika mji wa Chabahar kusini mashariki mwa Iran.
Taarifa iliyosomwa bungeni na mbunge wa Chabahar Yaqub Jadgal inasema: "Kwa mara nyingine ndugu zetu Mashia na Masuni wamekuwa wahanga wa njama za kikatili za madhalimu duniani ambao wana fikra potofu kuwa wanaweza kujikwamua kutoka kinamasi chao kwa kuzusha hitilafu katika nchi za Kiislamu ikiwemo Iran"
"Mrengo wa Masuni katika Majlisi unatuma salamu zake za rambirambi kwa taifa la Iran na familia za mashahidi. Ni matumaini yetu kuwa magaidi na mawakala wao ndani na nje ya nchi watatiwa nguvuni na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria"
Itakumbukwa kuwa mabomu yaliyotegwa na magaidi yaliripuka Jumatano iliyopita katika mjumuiko mkubwa wa waombolezaji wa mauaji ya Imam Hussein (as) katika mji wa Chabahar, kusini mashariki mwa Iran, na kuua na kujeruhi watu wasiopungua 110.
714514
captcha