IQNA

Tehran kuandaa kongamano la kwanza la wanafunzi wanaotetea Palestina

12:48 - January 12, 2011
Habari ID: 2063391
Kongamano la kwanza la Jumuiya ya Kimataifa ya Wanafunzi Wanaoitetea Palestina litafanyika Januari 17-19 mjini Tehran na kuwashirikisha wanafunzi na maafisa wa serikali kutoka nchi 50 duniani.
Hujjatul Islam Ali Akbar Safariipur, mkuu wa tawi la Iran la jumuiya huyo amesema kuwa: ‘Vituo na taasisi 50 kutoka nchi 50 duniani zimetangaza kuwa tayari kujiunga na jumuiyo hiyo na tayari wageni 120 wakiwemo wanafunzi na wakuu wa shule wametangaza kuwa tayari kushiriki katika kongamano hilo’.
‘Sherehe za ufunguzi zitahudhuriwa na Hamidreza Haji Babayi Waziri wa Elimu wa Iran, Ali Larijani Spika wa Bunge la Iran na Hujjatul Islam Mohammad Hassan Rahimian Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Taasisi ya Mashahidi na Masuala ya Maveterani’, ameongeza.
Afisa huyo amesema kongamano hilo la siku tatu litamalizika kwa hotuba ya Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Akbar Salehi.
Katika kongamano hilo pia kutanfayika uchaguzi wa bodi ya wakurugenzi na katibu mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wanafunzi Wanaoitetea Palestina.
727895
captcha