IQNA

IQNA Shirika bora zaidi la Habari

16:42 - January 24, 2011
Habari ID: 2069737
Shirika Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) limeteuliwa na kutangazwa kuwa shirika bora zaidi la habari katika warsha ya "Waqfu na Vyombo vya Habari" iliyofanyika Januari 23 mjini Tehran.
Warsha hiyo maalumu kwa vyombo vya habari vinavyotangaza masuala ya Kiislamu nchini Iran ilihudhuriwa na Ghulam Ali Haddad Adel Mkuu wa Tume ya Utamaduni katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge), Hujjatul Islam Muhammadi mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Shirika la Waqfu na Misaada na vilevile Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu anayeshughulikia masuala ya vyombo vya habari.
Mashirika ya Habari ya ISNA, IRNA na Fars yalichukua nafasi za pili, tatu na nne kwa taratibu.
Katika kitengo cha utangazaji na magazeti, magazeti ya Iran, Resalat, Kar-o-Karegar na Javan na vilevile kanali ya Qur'an na Qur'an FM yameshika nafasi za kwanza.
Katika warsha hiyo mwanaharakati mkongwe katika uga wa habari na mahusiano ya umma Kazemi Dinan alitunukiwa zawadi.
Hafla hiyo ilimalizika kwa hotuba na sala iliyosalishwa na mwanazuoni na mfasiri mashuhuri wa Qur'ani Sheikh Mohsen Qarati. 735188
captcha