IQNA

Ikhwanul Muslimin yampongeza Ayatullah Khamenei

11:53 - February 08, 2011
Habari ID: 2077115
Chama kikuu cha upinzani nchini Misri cha Ikhwanul Muslimin kimempongeza na kutoa shukrani za dhati kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullahi Ali Khamenei kwa kuunga mkono harakati za mapinduzi katika nchi za Misri na Tunisia.
Mwanachama mwandamizi wa chama hicho, Kamal Helbawi ametoa shukrani hizo kwa Ayatullah Khamenei kuhusu misimamo ya Ayatullah Khamenei aliyodhihirisha wazi katika hotuba za Swala ya Ijumaa ya wiki iliyopita mjini Tehran.
Mwanachama huyo wa Ikhwanul Muslimin ameipongeza hotuba ya Ijumaa iliyotolewa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema kuwa, ana matarajio makubwa kwamba harakati hizo za Wamisri zitazaa matunda hivi karibuni na taifa hilo la Kiarabu kupata serikali yenye kujali maslahi ya wananchi wake kama ya Iran.
Ayatullahi Khamenei alisema katika hotuba yake siku ya Ijumaa kuwa, Wamisri hawapiganii chochote kile ghairi ya hadhi na nafasi yao ambayo imekuwa ikikandamizwa na dikteta Hosni Mubarak, ambaye amekuwa kiongozi kikaragosi wa Marekani kwa zaidi ya miongo mitatu ya utawala wake.
Wakati huo huo, serikali ya Marekani imeanza kutuma manowari ya kivita, askari jeshi na silaha za kivita nchini Misri huku maandamano ya wananchi wa taifa hilo la Kaskazini mwa Afrika yakishika kasi zaidi. Hata hivyo, Pentagon imekanusha kuwa inaingilia kijeshi mgogoro wa kisiasa wa hivi sasa wa Misri na kujitetea kuwa, imechukua hatua hiyo ili kuandaa mazingira mazuri ya kuwasafirisha Wamarekani walioko nchini humo iwapo patakuwepo na haja ya kufanya hivyo.
Wamisri wanaandamana kwa siku ya 14 leo hii wakipinga utawala wa kiimla wa dikteta Hosni Mubara katika hali ambayo, mazungumzo kati ya serikali na upinzani yanaendelea. 743533
captcha