IQNA

Mkutano wa Umoja baina ya Waislamu katika Mtazamo wa Imam Khomeini wafanyika Zimbabwe

14:08 - February 20, 2011
Habari ID: 2083507
Mkutano wa Umoja baina ya Waislamu katika Mtazamo wa Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) ulifanyika jana katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.
Ofisi ya Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu ya Iran imeripoti kuwa maimamu 300 wa sala za Ijumaa na jamaa wa Zimbabwe wamehudhuria mkutano huo na kubadilishana mawazo kuhusu umuhimu wa kuwepo umoja na mashikamano baina ya Waislamu.
Mwambata wa Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Zimbabwe Asadi Muwahhidi amehutubia pia mkutano huo akizungumzia udharura wa kuwepo umoja na mashikamano baina ya Waislamu katika mtazamo wa Imam Khomeini na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei.
Maulamaa kadhaa wa Kiislamu wa Zimbabwe pia wamehutubia mkutano huo wakizungumzia umuhimu wa umoja baina ya Waislamu.
Mkutano huo pia umetumbuizwa kwa kasida na mashairi ya kumsifu Mtume Muhammad (saw). 749792


captcha