IQNA

Kiongozi Muadhamu akagua maonyesho ya teknolojia

9:15 - March 15, 2011
Habari ID: 2096048
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema jana alitembelea maonyesho ya teknolojia ya kistratijia na kukagua kwa karibu baadhi ya matunda muhimu ya sayansi na teknolojia ya wasomi wa hapa nchini.
Baada ya kuwasili katika maonyesho hayo ya teknolojia ya kistratijia, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu alielekea moja kwa moja katika eneo lililotengwa makhsusi kwa ajili ya kuwakumbuka mashahidi Ali Muhammadi na Dakta Shahriyari na kuwasomea al Fatiha na dua mashahidi hao wa sayansi na maarifa.
Katika maonyesho hayo kunaonyehwa uvumbuzi wa wasomi na wataalamu wa Iran kwenye medani za teknolojia ya anga, teknolojia ya mikroelektroniki, nishati jadidika, nano teknolojia, teknolojia ya mawasiliano, teknolojia ya seli shina na elimu ya tiba. 763863


captcha