Ameyasema hayo Jumatano asubuhi, Aprili 20, 2011, aliponana na maafisa na watafiti wa Kituo cha Nyaraka cha Mapinduzi ya Kiislamu.
Amesema kuwa, jambo linalopasa kupewa kipaumbele cha kwanza kabisa katika uandikaji wa historia ya Mapinduzi ya Kiislamu ni ubora na kuzingatia kuwa wanaotakiwa kusoma historia hiyo ni mamilioni ya vijana ambao hawana welewa wa kina kuhusu Mapinduzi ya Kiislamu na masuala yaliyokwenda sambamba na mapinduzi hayo.
Ameongeza kuwa, ni jambo muhimu mno kutumiwa historia kujaza pengo la uzoefu linalowakabili walengwa hasa kizazi cha vijana na kusisitiza kuwa, kama historia itahaririwa na kuandikwa kwa umakini wa hali ya juu na kwa njia sahihi, basi itawafanya watu wazidi kupata uzoefu na jamii nayo izidi kuelimika.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria masuala yanayohusiana na mapinduzi ya kupigania utawala wa katiba kama mfano mmoja wa matukio muhimu katika historia ya zama hizi ambayo yana uwanja mpana wa kupatia uzoefu na kukumbusha kuwa, mambo yaliyopelekea kutokea mapinduzi ya kupigania utawala wa katiba nchini Iran kama ilivyojiri kwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni tafakuri, fikra, malengo na matakwa ya wananchi ambao waliongozwa na mwanachuoni na kumwaga damu zao katika njia hiyo lakini cha kusikitisha ni kuwa mapinduzi ya kupigania utawala wa katiba yalipotoshwa na Waingereza kiasi kwamba baada ya kupita miaka 15 tangu yalipotokea mapinduzi hayo, ulianza utawala mweusi wa kidikteta wa kibaraka Reza Khan nchini Iran.
Ayatullah Udhma Khamenei amekumbusha kuwa, chanzo cha kudhihiri kipindi kichungu cha utawala wa Muhammad Reza Pahlavi nchini Iran wakati wa utawala wa katiba ni kupotoshwa mapinduzi ya wakati huo ya wananchi. Amesisitiza kuwa, ijapokuwa wimbi na harakati ya mapinduzi ya kupigania utawala wa katiba ilikuwa sawa na harakati ya wananchi iliyopelekea kupatikana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu lakini vipengee vya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran vimekwenda mbali zaidi na kuwa na kina kirefu zaidi ikilinganishwa na mapinduzi hayo ya kupigania utawala wa katiba.
Ameongeza kuwa, ni kwa sababu hiyo na ni kutokana na mwamko mkubwa wa kisiasa katika jamii na kupanuka mawasiliano ya kimataifa na mwamko mkubwa wa wanchii ndio maana tukasema kwamba kazi ya kuandika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran inatofautiana sana na kazi ya kuandika historia ya vitu vingine.
Ayatullah Udhma Khamenei amesema, kazi ya kuandika na kuhariri historia kama ya Mapinduzi adhimu ya Kiislamu ya Iran inahitajia umakini na ubora wa hali ya juu na kuongeza kuwa, kazi ya kuandika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu inabidi izingatie sana suala la namna ya uandishi, namna ya kupata habari sahihi, namna ya kuandika habari hizo na namna ya kuainisha vipaumbele katika taarifa na habari zenyewe.
Amesema taarifa zinazoandikwa katika historia inabidi ziwe na sifa ya kumkinaisha mlengwa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, kuwa na ratiba maalumu ya kuhariri vipaumbele katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu ni jambo la dharura sana na ameongeza kuwa, suala la kuainisha mlengwa nalo ni moja ya masuala muhimu katika uandishi wa historia ya Mapinduzi ya Kiislamu kwani mlengwa mkuu wa kazi hiyo ni kizazi cha vijana ambao hawana taarifa za kina kuhusu matukio ya Mapinduzi ya Kiislamu na wala malengo na matokeo ya mapinduzi hayo.
Ayatullah Udhma Khamenei amesema kuwa wananchi wa nchi nyinginezo ni walengwa wengine wa historia ya Mapinduzi ya Kiislamu na kusisitiza kuwa, watu walio wengi ulimwenguni kimsingi hawana taarifa za kina kuhusu historia ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran wakati ambapo kuna vitabu vingi na vizuri kuhusu mapinduzi mengine duniani vimeandikwa na kutarjumiwa.
Aidha amesisitizia umuhimu wa kuweko mawasiliano ya karibu baina ya Kituo cha Utafiti wa Nyaraka za Mapinduzi ya Kiislamu na waandishi wa vitabu, riwaya, wasanii na watu wanaotengeneza filamu za matukio ya kweli kuhusu mapinduzi na kusisitiza kuwa, leo hii watu wanaojishughulisha na sana ya kutengeneza sinema, watengenezaji filamu za matukio ya kweli na waandishi wa riwaya za kimapinduzi wako wengi nchini Iran na inabidi wasaidiwe na wapewe uungaji mkono mkubwa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitizia pia umuhimu wa kutumiwa vizuri mitandao ya Intaneti na kuongeza kuwa, kuweka mtandaoni nyaraka zenye taarifa sahihi na za kina kunaweza kuwasaidia sana watafiti katika kazi zao.
Ayatullah Udhma Khamenei vile vile ameashiria suala la kuandikwa kumbukumbu simulizi za historia ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa, miongoni mwa tatizo la kuandika historia inayotokana na maelezo ya maneno ya watu ni kuwa baadhi ya maelezo yanayotolewa si sahihi na baadhi ya wakati hutolewa fikra zilizopitwa na wakati na wakati mwingine hunuliwa mambo yasiyo na ukweli wowote na ambayo hayakuweko kabisa katika kipindi hicho cha historia badala ya matukio yake ya kweli.
Mwanzoni mwa mkutano huo, Hujjatul Islam Walmuslimin Husainiyan, Mkuu wa Kituo cha Nyaraka za Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, watafiti wa kituo hicho wanajitahidi sana kuhakikisha kuwa wanaielewa vilivyo historia ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuliakisi kwa watu tukio hilo adhimu bila ya upotofu wala mabadiliko yoyote.
Hujjatul Islam Walmuslimin Husainiyan ameashiria pia juhudi za Kituo cha Nyaraka za Mapinduzi ya Kiislamu za kuhakikisha kwamba kazi zake zote zinazofanywa na watafiti wake zinakuwa na ubora wa hali ya juu na kuongeza kuwa, ana matumaini kuwa kazi za kituo hicho zitakuwa marejeo makuu ya jamii ya kielimu na vijana.
778122