IQNA

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu asisitiza juu ya umuhimu wa sekta ya kilimo

14:11 - April 26, 2011
Habari ID: 2111976
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa sekta ya kilimo ni miongoni mwa sehemu muhimu mno na za daraja la kwanza hapa nchini kutokana na nafasi yake katika kudhamini usalama wa chakula na kuandaa nafasi za kazi.
Ayatullah Khamenei ameashiria nafasi ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) katika kutunga sheria zinazohitajika katika sekta ya kilimo na kusisitiza kuwa kuna udharura wa kuwepo ushirikiano mkubwa kati ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu na Serikali ili kuweza kufikia mtazamo mpana na wa kimsingi katika sekta ya kilimo. Ameongeza kuwa katika baadhi ya vipindi kulikuwepo fikra isiyosahihi kwamba mwelekeo wa Serikali unapaswa kutofautiana na kutengana na ule wa Bunge na kila moja kati ya nguzo hizo mbili za utawala inaona kujitawala kwake kuwa kumo katika kupinga upande mwingine. Amesisitiza kuwa masuala mbalimbali yanaweza kutatuliwa kwa ushirikiano na mtazamo wa pamoja wa Bunge la Serikali.
Akiashiria mpango wa kutoa ruzuku kwa uadilifu na hatua ya kutenga ruzuku ya serikali kwa sekta ya kilimo, Ayatullah Ali Khamenei amesema moja ya kazi kubwa na za kishujaa za serikali ya sasa ni hatua yake ya kutekeleza mpango wa kutoa ruzuku kwa uadilifu, na si sawa kudhoofisha hatua hiyo kwa kuashiria baadhi ya dosari za hapa na pale.
780869
captcha