Akizungumza kabla ya sala ya Ijumaa Mei 7 mjini Tehran, Hamid Haji Babaei aidha alisisitiza kuwa shule za kawaida kote nchini Iran zinapaswa kuchukua muelekeo kamili wa Qur’ani. Ameongeza kuwa vitabu vya shule pia vinapaswa kuandikwa kwa kuzingatia muelekeo kamili wa Qur’ani.
Ameashiria kumbukumbu ya kuuawa shahidi Ayatullah Murtadha Mutahhari ambayo huadhimishwa kama ‘Siku ya Mwalimu nchini Iran’ na kusema nafasi ya waalimu nchini ni ya kipekee.
Ameashiria hotuba ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu wiki iliyopita mbele ya hadhara kubwa ya waalimu na kusema: “Kama alivyoashiria Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Wizara ya Elimu ndio wizara muhimu zaidi ya serikali na kwamba uwekezaji wa kifedha na kimaanawi katika wizara hiyo bado hautoshi”.
Ameongeza kuwa Iran inapaswa kuwa na mfumo huru kabisa wa kielimu kwa msingi wa Kiislamu-Kiirani.
787408