"Ramadhani ni chimbuko la Qur'ani Tukufu na sisi katika ICRO tunajitahidi kuandaa programu mbalimbali za Kitabu Kitukufu kote duniani".
Dkt. Mohammad Bagher Khorramshad ameongeza kuwa, hivi karibuni, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliitaja Qur'ani kuwa nukta muhimu ya umoja, heshima na nguvu ya umma wa Kiislamu. 'Kwa hivyo katika mipango yetu tumezingatia kwa kina nafasi ya Qur'ani katika kuimarisha umoja wa Kiislamu'. Amesema 'Wiki ya Qur'ani' itafanyika katika nchi 20 za Asia, Afrika na Ulaya. Nchi hizo ni pamoja Sweden, Uingereza, Canada, Russia, Uturuki, Pakistan, Malaysia, Tunisia, Ufaransa na Kenya'.
836070