Amesisitiza kuwa taifa kubwa la Iran litafikia nafasi linayostahiki sambamba na kuwa na matumaini ya mustakbali mwema.
Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei aliyasema hayo alasiri ya jana katika kikao cha wanaharakati na wadau wa sekta binafsi, wakurugenzi wa masuala ya uchumi, viwanda, sekta ya kilimo, benki na huduma za jamii. Amesisitiza juu ya kufanyika bidii, kuwa na tadbiri na kasi kubwa zaidi katika kufikia malengo ya mpango wa ustawi wa taifa na kuongeza kuwa kumepatikana mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali hapa nchini kutokana na hima za shakhsia wa kielimu na masuala ya ufundi na kwamba fahari hii ya taifa inapaswa kuarifishwa kwa wananchi.
Akiashiria mashinikizo makali ya maadui dhidi ya Iran, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema lengo kuu la vikwao vya nchi za Magharibi ni kudumaza uchumi wa Iran. Amesema sababu kuu ya vikwazo hivyo si kadhia ya uzalishaji wa nishati ya nyuklia hapa nchini kwani vikwazo hivyo vilianza kutekelezwa dhidi ya Iran miaka 32 iliyopita hata kabla ya kuzungumziwa kadhia ya nyuklia hapa nchini.
Ayatullah Ali Khamenei amelitaka taifa na viongozi wa Iran kukabiliana kwa busara na vikwazo hivyo na akasema kuwa kama vikwazo hivyo vingekuwa na taathira na kukidhi matakwa ya maadui, vingetimiza malengo ya mabeberu katika miaka ya mwanzoni mwa Mapinduzi ya Kiislamu.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa kuzungumzia maendeleo hakuna maana ya kupuuza na kufumbia macho nakisi na udhaifu, na wakati huo huo kuzungumziwa nakisi na masuala hasi kunapaswa kufanyika kwa kutumia lugha ya kutia matumaini ili uhakika wa mambo katika Iran ya Kiislamu usidhihirishwe kinyume chake.
Ayatullah Khamenei amesema moja ya mbinu zinazotumiwa na maadui katika vita vya kisaikolojia katika kipindi cha sasa ni kuwavunja moyo na kuwakata matumaini wananchi hususan kizazi cha vijana na chenye nishati cha Iran; kwa msingi huo kuna udharura wa kueleza na kuakisi kwa wananchi maendeleo na uwezo mkubwa wa Iran. 845622