IQNA

Ayatullah Khamenei:

Siku ya Quds ni siku ya kimataifa ya Kiislamu

9:31 - August 25, 2011
Habari ID: 2176539
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa siku ya Kimataifa ya Quds ni siku ya Kimataifa ya Uislamu na kwamba matukio ya hivi karibuni katika Mashariki na Kati na kaskazini mwa Afrika ni ishara ya kufeli nadharia za kisiasa na kiuchumi za nchi za Magharibi.
Ayatullah Ali Khamenei ameyasema hayo katika hadhara ya mamia ya wahadhariri na viongozi wa vyuo vikuu waliokwenda kukutana naye na kuongeza kuwa Siku ya Quds ni siku kubwa na muhimu ambayo ndani yake taifa la Iran na mataifa mengine ya Kiislamu hupaza sauti ya haki ambayo ubeberu umewekeza kwa kipindi cha miaka sitini ili kuizima.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza matarajio kwamba mwaka huu pia Siku ya Kimataifa ya Quds itaadhimishwa ipasavyo katika nchi za Kiislamu. Ayatullah Khamenei amesema kuwa maendeleo ya kisayansi ni sehemu ya misingi na nguzo kuu za kusimama kidete na adhama ya taifa la Iran mbele ya kambi ya ubeberu na kuongeza kuwa maendeleo hayo ya kielimu na kisayansi ambayo yamelipa taifa la Iran hali ya kujiamini, fahari, azma kubwa, ushujaa na istiqama ni matokeo ya juhudi za vyuo vikuu, wahadhari na wanafunzi wa vyuo hivyo.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu pia ameashiria vitisho vya siku zote vya kijeshi, kiusalama, kijamii na kisiasa vya maadui, mauaji ya kigaidi yanayofanywa dhidi ya wasomi na vikwazo dhidi ya Iran na akasema, taifa la Iran limesimama kidete na kwa nguvu zote mbele ya kambi ya maadui na kusema “hapana” kwa mabeberu wanaotaka makuu wa kimataifa kwa kujiegameza kwenye maendeleo ya kisayansi na ya kivitendo ya nchi hii.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kufuta dini na elimu katika vyuo vikuu ni malengo mawili makuu ya kambi ya ubeberu. Ameongeza kuwa vijana wa Iran wanaoshikamana barabara na dini wameng’ara sana katika nyanja za utengeneszaji wa silaha za kijihami, seli shina, nishati ya nyuklia, teknolojia ya masuala ya anga, utengenezaji wa komputa kabambe na kadhalika na wanasonga mbele zaidi wakishirikiana na wasomi wengine hapa nchini.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia ameashiria hali ya sasa ya Mashariki na Kati na kaskazini mwa Afrika na akasema kuwa moja ya matunda ya matukio ya hivi sasa katika maeneo hayo ni kubainika vyema makosa ya nadharia za kisiasa na kiuchumi za Magharibi. Amesema kuwa matukio hayo na hali mbaya ya kiuchumi ya nchi za Magharibi kwa ujumla vinaonyesha kwamba nadharia za kisiasa na kiuchumi za Magharibi ni nakisi na gumba, kwa msingi huo tunapaswa kupiga hatua katika njia ya kuimarisha zaidi fikra na mitazamo ya Kiislamu. 849414



captcha