IQNA

Ayatullah Khamenei:

Kanali za Kizayuni zinafanya jitihada za kurembesha vigezo potofu

22:02 - October 18, 2011
Habari ID: 2207549
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa juhudi zinazofanywa na vyombo vya habari vya mfumo wa udikteta wa kimataifa kwa ajili ya kukuza na kurembesha vigezo potofu zimetolewa katika malengo hatari ya protokali za Wazayuni.
Ayatullah Ali Khameni ameyasema hayo leo katika hadhara ya wawakilishi wa taasisi mbalimbali za kielimu, kituamaduni, kiuchumi na Wasanii akiwa katika siku ya saba ya safari yake katika mkoa wa Kermanshah huko magharibi mwa Iran. Amesema kuwa huduma za kumfikisha mwanadamu katika ukamilifu ni lengo kuu la maendeleo na adhama ya mwanadamu. Ameashiria mwenendo wa madola ya kidhalimu na mabepari wa kimataifa wa kutumia vibaya elimu na sanaa na akasema kuwa Hollywood ambacho ni kituo kikuu cha filamu duniani, inatumiwa katika masuala ya kumporomosha mwanadamu na hisa ya mataifa kama Afghanistan na Iraq katika elimu ya nchi za Magharibi ni kupigwa mabomu na silaha za kemikali.
Ayatullahil Udhmaa Ali Khameni ameashiria siasa za miaka mingi za wakoloni za kuwadhalilisha wananchi wa Iran na kudai kwamba hawafai na akasema kuwa vijana na wasomi wa taifa la Iran wamebatilisha siasa hizo zilizodhidi ya Iran kwa maendeleo ya kustaajabisha ya sayansi na teknolojia katika kipindi cha miaka 32 ya baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria matokeo ya uchunguzi uliofanywa na vituo vya kimataifa unaothibitisha kwamba kasi ya ustawi wa kielimu nchini Iran ni mara kadhaa ikilinganishwa na wastani wa kimataifa na akasema kuwa, taifa la Iran litafungua nyanja mpya za sayansi na elimu mbele ya jamii ya wanadamu kwa kutegemea vipawa na kujiamini kwa vijana wake.
Vilevile amekumbusha historia na mirathi iliyojaa fahari ya kiutamaduni ya Iran na kusema kuwa katika zama ambapo nchi za Magharibi zilikuwa katika giza totoro la kielimu, Iran ilikuwa mstari wa mbele wa elimu kati ya nchi za Kiislamu.
Ayatullahil Udhmaa Khamenei ameitaja elimu na sanaa kuwa ni hiba ya Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu na akaongeza kuwa taifa la Iran na Jamhuri ya Kiislamu litatumia hiba hiyo katika kuhudumia Uislamu, masuala ya kiroho na kwa ajili ya kustawisha na kumkamilisha mwanadamu. 882301


captcha