IQNA

Iran yaonya kuhusu njama za wabeberu za kuzusha hitilafu kati ya Suni na Shia

10:09 - March 07, 2012
Habari ID: 2287144
Ali Larijani Spika wa Majlisi (Bunge) ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuzusha hitilafu na mifarakano kati ya madhehebu ya Shia na Suni ni moja ya malengo ya machafu Uistikbari wa dunia ya kuitenga Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Lariani amesistiza juu ya juhudi zinazofanywa na Iran za kuleta umoja baina ya wafuasi wa madhehebu ya Shia na Suni. Dakta Ali Larijani ameyasema hayo Jumanne mjini Tehran alipohutubia katika kikao cha Baraza la Wanazuoni Wanaomchagua Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusimamia kazi zake.
Spika Larijani amesema, stratejia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuamiliana na masuala yanayohusu eneo zinatekelezwa kwa welewa na umakini mkubwa pamoja na maamuzi ya busara ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Akitoa uchambuzi kuhusiana na hali ya uchumi wa Iran, Dakta Ali Larijani amesema bayana kwamba, licha ya kuwepo vikwazo na mashinikizo ya Wagharibi dhidi ya taifa la Iran, uchumi wa nchi hii upo katika hali nzuri, ya kuridhisha na ya ustawi.
966640
captcha