IQNA

Khatibu wa Ijumaa Tehran:

Kulisaidia taifa la Syria ndio msingi wa mapambano dhidi ya mashambulizi ya Uzayuni

12:17 - April 01, 2012
Habari ID: 2296137
Hatibu wa sala ya Ijumaa mjini Tehran ameyasifu matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran aliyoyasema katika kikao na Waziri Mkuu wa Uturuki kuhusiana na hali ya mambo nchini Syria na kuyataja kuwa yenye umuhimu mkubwa.
Hujjatul-Islam Walmuslimin Kadhim Sidiqi amesema kuwa, sisitizo la Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran la kulisaidia taifa la Syria ndio msingi wa mapambano dhidi ya mashambulizi ya uzayuni kwa manufaa ya nchi zote za Mashariki ya Kati. Aidha khatibu wa sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesifu hatua ya kufanyika kikao cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu mjini Baghdad na kusema huo ni ushindi mkubwa kwa taifa hilo. Amesema hilo limewathibitishia walimwengu kuwa baada ya kuondoka vikosi vamizi nchini humo, jeshi la nchi hiyo linao uwezo wa kulinda amani ya nchi hiyo lenyewe. Katika hatua nyingine Hujjatul-Islam Walmuslimin Kadhim Sidiqi amepongeza kauli ya jumuiya hiyo ya Kiarabu ya kuunga mkono juhudi za Tehran za kustafidi na mipango yake ya nyuklia kwa malengo ya amani na vilevile uungaji mkono wake kwa suala zima la Palestina na kupambana na ugaidi.
976435
captcha