IQNA

Mwanafikra wa Lebanon:

Kuwasaidia watu wanaodhulimiwa kote duniani ni statijia ya Iran ya Kiislamu

21:11 - April 04, 2012
Habari ID: 2298137
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaendelea kusisitiza na kushikamana barabara na misimamo yake ya kimsingi na kistratijia ya kuyahami mataifa yanayokandamizwa na kudhulumiwa kote duniani ambayo ilianzishwa na hayati Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu.
Hayo yamesemwa na mwanafikra wa Lebanon ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Qauluna Wal-amal Sheikh Ahmad Qatan. Ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ingali inashikamana barabara na sera zake za kupigania haki za taifa la Iran na mataifa mengine yanayodhulumiwa mbele ya mabeberu.
Amesema misimamo imara ya kupinga sera za Marekani ya Iran inatokana na sera za kimsingi na kistratijia za nchi hiyo za kuwatetea watu na mataifa yanayokandamizwa na kudhulumiwa.
Sheikh Al Qatan amesema kuwa hotuba iliyotolewa siku chache zilizopita na Ayatullah Ali Khamenei inatofautiana kikamilifu na matamshi ya viongozi wa nchi za Kiarabu ambao wanajisalimisha kwa Wamagharibi.
Amesema katika hotuba yake Ayatullah Khamenei- kama ilivyo kawaida yake- amezungumzia masuala ya mataifa yanayokandamizwa na maslahi yao kama alivyozungumzia maslahi ya Iran, na mtazamo wake unapita mipaka ya kijiografia ya Iran.
Sheikh al Qatan amesema hotuba ya siku chache zilizopita ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ilikuwa na ujumbe muhimu kwa maadui wa Iran na wale wote wanaofikiria kufanya njama dhidi ya nchi hiyo. 978654

captcha