IQNA

'Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo ina nafasi muhimu Iran'

14:59 - April 09, 2012
Habari ID: 2300934
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, baadhi ya masuala muhimu ya nchi yanatatuliwa na Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu na kwamba Halmashauri hiyo ina nafasi muhimu mno katika serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, baadhi ya masuala muhimu ya nchi yanatatuliwa na Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu na kwamba Halmashauri hiyo ina nafasi muhimu mno katika serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Ayatullahil Udhma Khamenei amesema hayo katika mazungumzo na mkuu na wajumbe wa duru mpya ya Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu nchini Iran, na kuongeza kuwa, halmashauri hiyo ni dhihirisho la jinsi busara na hekima zinavyofanya kazi kwa pamoja katika mfumo wa Kiislamu nchini Iran. Vile vile ameagiza kuwa, maslahi ambayo yanaainishwa na halmashauri hiyo lazima yawe yanakubaliwa na wajumbe wengi sambamba na kuaminika kuwa ni yenye maslahi kwa jamii.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiaria majukumu ya Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu kama yalivyotajwa katika katiba na kuongeza kuwa, kumshauri Kiongozi kwa ajili ya kuainisha siasa kuu za dola ya Kiislamu na kuratibu siasa hizo ambazo kwa hakika ndio msingi wa sera za mihimili mikuu ya Dola (yaani Bunge Serikali na Mahakama) ni moja ya kazi zenye umuhimu wa juu kabisa za Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu nchini Iran.
981217
captcha