IQNA

Ayatullah Khamenei:

Kuwaridhisha wananchi huvuta radhi za Mwenyezi Mungu

0:25 - April 16, 2012
Habari ID: 2305472
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei adhuhuri ya leo Jumapili amehutubia hadhara iliyojumuisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah), makamanda wa jeshi la polisi na wafanyakazi wa jeshi hilo na kusisitiza kuwa kuwaridhisha wananchi humfanya mwanadamu apate radhi za Mwenyezi Mungu.
Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa iwapo viongozi wa nchi wataweza kuzipa utulivu nyoyo za wananchi, hapana shaka kuwa watapata radhi za Mwenyezi Mungu.
Amewataja maafisa wa jeshi la polisi hapa nchini kuwa ni askari wa mfumo wa Kiislamu na kusisitiza kuwa, suala la kudhamini usalama ni miongoni mwa haja kubwa na utangulizi unaotayarisha uwanja mzuri wa kubuni mipango mbalimbali. Amesema kuwa, kama hakuna usalama na amani katika jamii hakuna kazi yoyote inayoweza kufanyika kwa mpangilio mzuri kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa nchi.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza juu ya udharura wa kuwepo mipango mizuri na ya busara ya jamii, bidii kubwa na muamala mwema kwa ajili ya maendeleo na harakati ya kusonga mbele taifa. Amesema kuwa sharti la kutekelezwa na kutimizwa mipango mbalimbali ni kudhaminiwa usalama na amani katika jamii.
Ameashiria baadhi ya matatizo ya mtu binafsi na ya jamii na kusema: “Kama ambavyo mtu binafsi yumkini akakumbwa na matatizo ya kinafsi na kiroho, jumuiya na taasisi mbalimbali pia zinaweza kupatwa na matatizo ya ufisadi; kwa msingi huo kuna udharura wa kuwa macho na makini katika kukabiliana na hali hiyo.”
Ayatullah Ali Khamenei amesisitiza kuwa moja ya mambo yanayotayarisha uwanja mzuri wa kupatikana maendeleo ya nchi ni kuzingatia uaminifu, ukweli, kushikamana na dini na kutekeleza vyema majukumu na pia kuweka mbele maslahi ya jamii kuliko maslahi ya mtu binafsi. Amesema kuwa jamii inayokuwa na watu wanaofanya kazi kwa moyo wa aina hii hufika kwenye kilele cha maendeleo na kupata nguvu na uwezo wa kudumu.
Mwanzoni mwa mkutano huo na kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Kamanda wa Jeshi la Polisi la Iran Meja Jenerali Ahmadi Muqaddam alitoa ripoti kuhusu utendaji wa jeshi hilo katika kupunguza jinai na uhalifu, uvumbuzi wa dawa zaidi za kulevya, mafanikio ya jeshi hilo katika maeneo ya mipakani, kupungua kwa ajali za barabarani, kuongezeka huduma za jeshi la polisi kwa wananchi na kuridhishwa wananch na kazi inayofanywa na jeshi hilo. 986468
captcha