IQNA

Mwamko wa Kiislamu ni natija ya fikra za Imam Khomeini MA na Imam Khamenei

12:16 - May 14, 2012
Habari ID: 2325446
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu amesema moja ya mafanikio makubwa ya hayati Imam Khomeini MA na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Imam Khamenei ni kutoa mwelekeo kwa mwamko wa Kiislamu.
Akizungumza Jumapili katika kongamano la 'Nadharia ya Mwamko wa Kiislamu Katika Fikra za Kisiasa za Imam Khomeini MA na Imam Khamenei', Ayatullah Tashiri ameongeza kuwa nafasi kubwa ya Imam Khomeini katika ustawi wa Mwamko wa Kiislamu duniani ndio sababu iliyopelekea madola ya istikbari duniani kumpinga.
Amesema Mapinduzi ya Kiislamu Iran yaliamsha hisiasa za watu wenye fikra huru na kuyaletea wasi wasi madola makubwa yenye kiburi.
Mwanazuoni huyo wa ngazi za juu amesema kuwa Mapinduzi ya Kiislamu yamevunja njama na mipango ya Wamagharibi katika eneo.
Amemnukulu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyesema kuwa katika nusu ya kwanza ya karne ya 20, madola ya kibeberu yalikuwa yameudhibiti ulimwengu wa Kiislamu yakiwa na malengo matatu ya kuibua mifarakano katika nchi za Kiislamu, kuzibakisha nyuma nchi za Kiislamu na kueneza usekula lakini kwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, njama hizo zote zilifeli.
1007068
captcha