IQNA

Uungaji mkono wa Imam Khamenei kwa watu wa Bahrain wapongezwa

13:10 - June 05, 2012
Habari ID: 2340378
Muungano wa Februari 14 wa Bahrain umetoa taarifa na kumshukuru kwa dhati Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Imam Sayyed Ali Khamenei kwa uungaji mkono wake kwa mapinduzi ya Bahrain.
Katika taarifa Muungano wa Februari 14 wa Bahrain umeashiria hotuba ya Imam Khamenei Siku ya Jumapili alipohutubia umati mkubwa kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 23 wa kurejea kwa mola wake Imam Khomeini (quddisa sirruh) muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Muungano huo umesema: 'Kwa mara nyingine Imam Khamenei ameunga mkono mataifa yanayodhulumiwa katika ulimwengu wa Kiarabu na wananchi wachukue tahadhari ili maadui wasite mwamko wa Kiislamu na mapinduzi ya umma.
Katika hotuba ya yake Imam Khamenei alisema : 'Wananchi wa Bahrain wanakandamizwa na utawala wa kiimla na kidikteta bila ya sababu yoyote na upinzani wa wananchi hao unajibiwa kwa vitendo vya kikatili kabisa wakati ambapo wananchi wa Bahrain hawapiganii kitu kingine isipokuwa haki yao ya kimsingi kabisa yaani demokrasia na kuwa na maamuzi katika nchi yao.
Aidha Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran alisema badala ya kusikilizwa matakwa ya wananchi huko Bahrani, kunafanyika njama za kulipa sura ya hitilafu za kimadhehebu suala la nchi hiyo na kulihusisha na Ushia na Usuni sambamba na kuficha matakwa halisi ya wananchi wa nchi hiyo.
Muungano wa Februari 14 wa Bahrain umelaani uingiliaji wa utawala wa Marekani nchini humo na vile vile kukosoa vikali hatua ya vikosi vya ufalme wa Saudia kukali kwa mabavu ardhi ya Bahrain.
Aidha wanamapinduzi hao wa Bahrain wamesema mapinduzi yao yamepuuzwa na vyombo vya habari vya Kimagharibi duniani ambavyo vinaficha jinai na ukatili wa utawala wa Aal Khalifa katika nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.
1023033
captcha