IQNA

Kalamu na simu ya mkononi ya Qur'ani yaanza kuuzwa India

21:27 - July 07, 2012
Habari ID: 2362860
Kalamu ya elektroniki na simu ya mkononi makshsusi kwa ajili ya kusoma Qur'ani Tukufu vimeanza kuuzwa nchini India kwa mnasaba wa kukaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa ajili ya kutayarisha uwanja mzuri kwa wasomaji wa kitabu hicho.
Kituo cha habari cha The Hindu kimeripoti kuwa utumiaji wa kalamu na simu hiyo ya mkononi unamuwezesha mtumiaji kusoma matini ya sura za Qur'ani, tarjumi ya kitabu hicho kwa lugha 19 tofauti na kusikiliza kiraa ya Qur'ani ya makarii na wasomaji 16 mashuhuri duniani.
Kalamu na simu hiyo ambavyo vimetengenezwa nchini Uchina vimeanza kuuzwa katika mji wa Bombay na miji mingine kadhaa ya India.
Simu na kalamu hiyo vinamuwezesha mmiliki kusoma tafsiri na tarjumi za Qur'ani kwa lugha kama Kiingereza, Kiurdu, Bengali, Malai, Tamil, Pashtu, Kifarsi, Dari, Kituruki, Kifaransa, Kijerumani, Kirussia na Kichina.
Mbali na hayo kalamu na simu hiyo pia vina vitabu 33 vya maudhui mbalimbali za Kiislamu, adhana, matangazo ya wakati wa kisheria wa swala, uwezo wa kuainisha upande wa kibla na kadhalika. 1046996


captcha