IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu:

Kimya cha Magharibi mbele ya mauaji yanayofanywa dhidi ya Waislamu Myanmar ni kielelezo cha urongo wa madai yao ya kutetea haki za binadamu

15:38 - July 22, 2012
Habari ID: 2374793
Sambamba na siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi ambao Qur'ani Tukufu iliteremshwa dnani yake, alasiri ya jana Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alishiriki katika najlisi ya kiraa ya Qur'ani iliyoshirikisha makarii na mahafidhi wa kitabu hicho kitukufu.
Wasomaji na makarii hao walitia nuru majlisi hiyo kwa kiraa ya aya za Qur'ani na baadaye makundi mbalimbali yaliimba qasida na kusoma tungo za kusifu mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Ayatullah Ali Khamenei alihutubia majlisi hiyo akisema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatoa wito wa kuasisiwa ustaarabu uliojengeka juu ya misingi ya masuala ya kiroho yanayobainishwa kwenye Qur'ani Tukufu na uongozi wa Mola Muumba. Ameashiria unyonyaji unaofanyika dhidi ya wanadamu katika ustaarabu wa Magharibi uliojengeka juu ya misingi ya maada na uliombali na maadili na masuala ya kiroho na akasema: "Kielelezo cha wazi zaidi cha madai ya uongo ya Magharibi kuhusu maadili na haki za binadamu ni kunyamaza kimya kwa nchi zinazodai kushika bendera ya kutetea haki za binadamu mbele ya mauaji yanayofanywa dhidi ya Waislamu huko Myanmar.
Ayatullah Khamenei amesema kuwa kila mahala ustaarabu wa Magharibi ulipotia mguu wake katika karne zilizopita matokeo yake yalikuwa ni ufisadi na kuwanyonya wanadamu.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema izza, hali bora, maendeleo ya kimaada na kimaanawi, maadili na ushindi dhidi ya maadui vinapatikana tu kupitia njia ya kutekeleza kivitendo maarifa ya Qur'ani Tukufu.
Amesisitiza juu ya udharura wa kuambatanishwa akili na hisia katika kuanisika na Qur'ani Tukufu na akasema kuwa wakati itikadi za kiakili na kimantiki za Qur'ani zinapochanganyika na upendo na mahaba hutayarisha uwanja wa kutekelezwa mafundisho ya Qur'ani, na matokeo yake ni kuongezeka taufiki ya jamii ya Kiislamu.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza kufurahishwa na kasi ya kuenea harakati ya kuanisika na Qur'ani hapa nchini hususan kati ya tabaka la vijana na akasisitiza juu ya udharura wa kutadabari na kutafakari katika maana ya aya za Qur'ani tukufu na kuyafanyika kazi. 1058835


captcha