IQNA

Kiongozi Muadhamu:

Mashairi yanapaswa kutumiwa katika kuhudumia dini, maadili na harakati ya kimapinduzi ya taifa

15:26 - August 05, 2012
Habari ID: 2386087
Sambamba na maadhimisho ya siku ya kuzaliwa mjukuu wa Mtume Muhammad (saw), Imam Hassan bin Ali bin Abi Twalib (as) Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei jioni ya leo amehutubia hadhara ya walimu wa lugha na fasihi na Kifarsi na washairi vijana waliokwenda kuonana nae.
Amesema msafara wa mashairi hapa nchini unasonga mbele kwa kasi, umakini na mwelekeo mwema na kuongeza kuwa kutokana na kuendelea harakati hiyo, nchi azizi ya Iran itautunuku tena ustaarabu na utamaduni wa dunia hususan eneo hili la Mashariki ya Kati hadia yenye thamani.
Ayatullah Khamenei amesema mbali na mashairi kuwa chombo kinachobainisha hisia za kishairi na kuhudumia thamani, mshairi pia anapaswa kutumia neema hiyo kubwa ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuhudumia dini, maadili, mapinduzi na kuzidisha maarifa.
Amesisitiza juu ya kutiliwa maanani maana na madhmuni ya mashairi sambamba na hisi za kishairi na akasema kuwa mashairi yanaweza kutoa huduma kwa maarifa ya kidini, maadili ya wananchi na harakati ya kimapinduzi ya taifa na suala hilo linawezekana hata kwa beti moja mbili za shairi la kimapinduzi, kimaadili au lenye maarifa ya kidini.
Ayatullah Khamenei amesisitiza juu ya umuhimu wa nguzo tatu muhimu ambazo ni neno linalofaa, wazo au madhumuni na hisia nyepesi za kishairi na akaongeza kuwa, mashairi hayawezi kupuuza na kufumbia macho masuala yanayotawala jamii ya sasa hapa nchini.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema dhulma kubwa inayofanywa dhidi ya Iran katika sekta ya nishati ya nyuklia na mauaji dhidi ya wasomi hapa nchini ni mfano wa masuala yanayojiri kwa sasa hapa nchini. Ameongeza kuwa kambi ya ubeberu imesisimama kwa ukhabithi kamili mkabala wa taifa la Iran kwa nguvu zote za kipropaganda na uwezo wake wote wa kisaisa, na taifa letu linapambana; suala hili la kitaifa halipaswi kufumbiwa macho na mshairi anayeshikamana na dini, kwani haiwezekani kutokuwa na upande wowote wakati wa mpambano baina ya haki na batili.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekumbusha misimamo ya baadhi ya watu waliojiita wazalengo na wapenda nchi yao kuhusu masuala ya vita vya kulazimishwa na uvamizi wa adui dhidi ya Iran na akasema kuwa, watu hao wanahubiri suala la kutojali, kutoheshimu sheria za dini na kutojali maadili na masuala muhimu ya nchi na Mapinduzi ya Kiislamu na wakati huo huo hawakuchukua msimamo wowote kuhusu suala la kushikamana na maadui.
Mwishoni mwa hotuba yake Ayatullah Ali Khamenei ametoa nasaha akisema wale wanaowekeza rasilimali yao ya sanaa katika upande wa kambi ya haki na masuala ya kiroho wanapaswa kuwa macho daima na kusimama kidete katika njia ya haki.
Mwanzoni mwa kikao hicho washairi kadhaa walisoma tungo zao zenye malengo ya kidini, kimapinduzi, kijamii na mwamko wa Kiislamu. 1070961


captcha