IQNA

Nakala za kale za Qur'ani zaonyeshwa Kashmir

18:37 - August 14, 2012
Habari ID: 2393074
Maonyesho ya nakala za kale zilizoandikwa kwa hati za mkono za Qur'ani Tukufu yanafanyika katika Akademia ya Sanaa, Utamaduni na Lugha Mbalimbali katika mji wa Srinagar kwenye jimbo la Jamu na Kashmin.
Maonyesho hayo yamefunguliwa na Waziri Mkuu wa jimbo la Jamu na Kashmir Umar Abdullah na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa wa ngazi za juu wa jimbo hilo.
Baada ya kukagua maonyesho hayo Waziri Mkuu wa Jimbo la Kashmir aliandika katika daftari la watu waliotembelea maonyesho hayo kwamba: "Ni Wajibu wetu kulinda na kuhifadhi hazina ya nakala za kale za Qur'ani kwa ajili ya kizazi kijacho."
Vilevile alitoa zawadi ya bajeti ya kuzitia katika muundo wa dijitali nakala hizo za kale za Qur'ani Tukufu.
Katika maonyesho hayo kunaonyeshwa nakala 100 za kale za Qur'ani Tukufu zilizoandikwa kwa hati za mkono ikiwemo ile ya Fat-hullah Kashmiri ambayo iliandikwa zaidi ya miaka 700 iliyopita.
Katika upande wa tafsiri kunaonyeshwa tafsiri ya al Kash-shaf ya Allamah Zamakhshari iliyoandikwa katika karne ya 12 ambayo ilipelekwa Kashmir na mtawala wa wakati huo wa eneo hilo Zainul Abidin kutoka Makka, Tafsiri Kabir iliyochapishwa karne ya 12, Jawahirul Tafsiri ya Allamah Tantawi na tafsiri ya Baidhawi zilizochapishwa katika karne ya 14.
Katika maonyesho hayo pia kuna muhuri uliokuwa ukitumiwa na Mtume Muhammad (saw), barua yake kwa mtawala wa Iran akimlingania Uislamu, barua ya Nabii Sulaiman kwa Malkia wa Sheba na aya za kwanza za Qur'ani zilizoandikwa kwenye mifupa ya ngamia. 1078687
captcha