IQNA

Katika mazungumzo yake na Rais wa Mongolia:

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu asisitiza juu ya kuimarishwa ushirikiano wa kiuchumi, kielimu na kiutamaduni

0:49 - September 02, 2012
Habari ID: 2402866
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ameonana na na kufanya mazungumzo na Rais Tsakhiagiin Elbegdorj wa Mongolia. Ayatullah Khamenei amezungumzia masuala ya kihistoriaa na kiutamaduni yanayozikutanisha pamoja Iran na Mongolia ikiwa ni pamoja na athari za kihistoria na kielimu za kipindi cha utawala wa Wamongoli nchini Iran na akasema kuwa, uhusiano wa Iran na Mongolia unapaswa kupanuliwa zaidi kwa kutilia maanani historia hiyo.
Ameutaja uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni mkubwa na kusisitiza kuwa, nchi mbili hizi zinaweza kuwa na ushirikiano mpana zaidi katika nyanja za masuala ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, vyuo vikuu na katika masuala ya kimataifa.
Kwa upande wake Rais wa Mongolia amesema masuala ya kihistoria na kiutamaduni yanayozikutanisha pamoja nchi hizi mbili ni uwanja mzuri kwa ajili ya kustawisha uhusiano wa pande mbili. Ameongeza kuwa Mongolia ina hamu kubwa ya kuimarisha uhusiano wake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa ni pamoja na katika masuala ya kiuchumi, kisiasa, miundombinu na kubadilishana wanafunzi na wahadhiri wa vyuo vikuu.
Rais wa Mongolia amesisitiza kuwa anakubaliana na mitazamo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu Mashariki ya Kati isiyokuwa na silaha za nyuklia na kwamba utumiaji wa nishati ya nyuklia kwa matumizi ya kiraia ni haki ya nchi zote. 1089002

captcha