IQNA

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu:

NAM inapaswa kutumiwa kwa ajili ya kuzuia mashinikizo ya madola ya kidhalimu dhidi ya nchi huru

0:50 - September 02, 2012
Habari ID: 2402868
Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo amefanya mazungumzo na Rais Sheriff Namajo wa Guinea Bissau na kusema kuwa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) ni chombo bora kwa ajili ya ushirikiano wa aina mbalimbali kati ya nchi wanachama.
Amesema kuwa iwapo wanachama wa jumuiya hiyo zitakuwa na ushirikiano mkubwa katika fremu ya NAM, hapana shaka kwamba jitihada za madola ya kidhalimu za kuyawekea vikwazo na mashinikizo nchi zinazojitawala zitaambulia patupu.
Amesisitiza kuwa sharti la kuwepo ushirikiano mkubwa wa nchi wanachama wa NAM ni kuanzishwa taasisi madhubuti za utendaji na kuongeza kuwa, madola ya kibeberu yanaeneza propaganda kwamba haiwezekani kusimama kidete mbele yao, lakini wananchama wa jumuiya ya NAM wanaweza kuthibitisha kinyume cha madai hayo ya kipropaganda.
Katika mazungumzo hayo Rais Sheriff Namajo wa Guinea Bissau ameeleza hamu ya nchi yake ya kustawisha zaidi uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyanja mbalimbali. 1089005

captcha