IQNA

Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Iran:

Jeshi la Iran litawashinda maadui

0:01 - September 19, 2012
Habari ID: 2414736
Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa jeshi hilo kupata uwezo mkubwa wa kuzuia aina yoyote ya mashambulizi ya adui dhidi ya Iran ya Kiislamu.
Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei ambaye alikuwa akihutubia hadhara ya makamanda wa jeshi la Iran na watayarishaji wa maonyesho ya mafanikio ya jeshi hilo katika mji wa Noushahr huko kaskazini mwa Iran, ameelezea kuridhishwa kwake na maendeleo makubwa ya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu na kusisitiza kuwa jeshi hilo linapaswa kupata uwezo mkubwa ambao hautampa mtu yeyote nafasi ya kushambulia ngome imara ya nchi na taifa la Iran.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa kuambatanishwa elimu na vitendo ndio sababu muhimu zaidi ya kufikiwa malengo na kutekelezwa kazi kwa njia sahihi. Amelitaka jeshi la Iran kutilia maamani suala hilo muhimu.
Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei ameashiria sisitizo la mafundisho ya Uislamu kuhusu nafasi ya juu ya elimu na amali na udharura wa kuambatanishwa viwili hivyo na kusema: "Kama ilivyosisitizwa tangu miaka mingi iliyopita, vituo vya elimu na mafunzo katika vikosi vya jeshi vinapaswa kuwa na maendeleo na ustawi endelevu.
Amiri Jeshi Mkuu amesema kuwa lengo la muda mrefu la majeshi ya Iran ni kuwa na jeshi imara na linaooana na malengo na thamani za Jamhuri ya Kiislamu. Ameongeza kuwa thamani na malengo ya utawala wa Kiislamu hapa nchini ni mapana na yanahusu jamii nzima ya binadamu na haijuzu kushambulia na kuvunja heshima na mamlaka ya nchi yoyote kwa ajili ya kutimiza malengo hayo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amelitaka jeshi kutoa kipaumbele kwa sayansi na elimu ya kisasa, kudumisha utengenezaji wa zana za kijeshi, kuzidisha kasi ya harakati ya utengenezaji vipuri, kuboresha na kubuni vitu vipya katika medani ya sayansi, kutumia walimu hodari, kupanua zaidi ushirikiano na vituo vya elimu na sayansi na vyuo vikuu na kutilia maanani masuala ya kimaanawi na kiroho. 1101831
captcha