IQNA

Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Kikao cha Sala

13:19 - January 01, 2015
Habari ID: 2663165
Kikao cha 23 kikuu cha Sala nchini Iran kimefunguliwa Jumatano kwa ujumbe wa Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mjini Ahwaz (kusini magharibi mwa Iran).

Matini kamili ya ujumbe huo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambao umesomwa katika kikao hicho na Hujjatul Islam Walmuslimin Qarati, mkuu wa kamati ya kusimamisha Sala nchini Iran, ni kama ifuatavyo:


Bismillahir Rahmanir Rahim
Kwa miaka mingi sasa na kwa hima na jitihada zilizojaa baraka za miaka yote hii, nyoyo na fikra za watu nchini zinazidi kunawirishwa na kikao hiki ambacho kinazifanya nyoyo na fikra za watu zizidi kuizingatia na kuipa umuhimu ibada ya Sala na kueneza mambo mazuri, kumbukumbu nzuri na maonyo mbali mbali kuhusiana na faradhi hiyo isiyo na mfano wake katika Uislamu na nguzo hiyo madhubuti ya dini na kushikamana na mafundisho ya kidini. Hii ni taufiki kubwa kwenu nyinyi waendeshaji wa kikao hiki na ni atia nzuri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili yetu sisi tunaofuatilia na kufaidika na kikao hiki.
Hivi sasa umewadia wakati wa kutathminiwa matunda ya jitihada hizi zenye thamani kubwa na faida zake kwa kufanya utafiti wa kina wa kuangalia mambo katika uhalisia wake iwe ni katika vitendo na mienendo ya walengwa ambao wamelengwa kwenye ripoti ya Sala na kuusiwa kutekeleza vilivyo ibada ya Sala na kutoidharau hata kidogo, hususan vijana na wale wote waliofikia baleghe ya kuwajibikiwa na Sala, au iwe ni upande wa kuchunguza kutekeleza kwa njia sahihi ibada ya Sala na kwa unyenyekevu mkubwa pamoja na kuuhudhurisha moyo pamoja na kuzingatia vitu vya asili vya amali hiyo njema iliyojaa rehema za Mwenyezi Mungu. Iwe ni katika kuelewa wajibu wa kutekeleza ipasavyo majukumu yao watu ambao wamewadhifishwa na kupewa fursa ya kusimamia suala hilo la Sala, kama vile ujenzi, usimamiaji na uendeshaji wa misikiti, au kuandaa na kuratibu utekelezaji wa Sala katika mashule na Vyuo Vikuu, au kuandaa fursa za kuweza Waislamu kusali wanapokuwa katika safari za nchi kavu na angani au kutumia mbinu za sanaa katika kueneza utekelezaji wa ibada tukufu ya Sala kama vile kupitia vyombo vya mawasiliano ya umma kama vile video na vyombo vya sauti au kuzalisha makala na vitabu vinavyobainisha ubora wa ibada hii inayochukua muda mfupi kuitekeleza lakini yenye faida kubwa na... au iwe ni katika nyuga nyinginezo ambazo majukumu ya utekelezaji wake wamekabidhiwa watu maalumu kusimamia utekelezaji wake.
Kufanyika kikao cha Sala ni hatua iliyojaa baraka, ni jambo muhimu na bila ya shaka ni hatua yenye ujira mzuri kutoka kwa Mwenyezi Mungu, lakini ili jambo hilo lenye thamani liweze kufanikiwa na kuzidi kufikia kwenye nukta ya ukamilifu na kwenye faida zilizokusudiwa, inabidi kazi hiyo ifanyiwe tathmini kwa muono wa kina wa kuangalia uhalisia wa mambo, kwa busara na kufuatiliwa kwa karibu matunda yake. Kufanya hivyo ni sehemu muhimu sana katika ubunifu huu (wa kuitisha vikao vya Sala).
Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu akupeni nyote taufiki hususan mwanachuoni azizi na mwenye hadhi, Hujjatul Islam Walmuslimin, Janab Qarati.

Sayyid Ali Khamenei,
9 Dei 1393
(Disema 30, 2014).

2657683

captcha