IQNA

Kiongozi Muadhamu: Kadhia ya Palestina ni muhimu zaidi

16:23 - January 27, 2015
Habari ID: 2770295
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kadhia ya Palestina ndiyo yenye umuhimu mkubwa zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kusimama kidete hadi pale malengo ya Palestina yatakapotimia na hapana shaka kuwa vijana watashuhudia siku hiyo.

Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei ameyasema hayo Jumatatu mjini Tehran katika mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Palestina, Ahmad Jibril. Amepongeza huduma na juhudi kubwa za Katibu Mkuu wa harakati hiyo katika njia ya kupigania malengo ya Wapalestina na akasema: Ahmad Jibril ni miongoni mwa nguzo muhimu za kadhia ya Palestina.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza matarajia kwamba mapambano ya Palestina yataendelea hadi utakapopatikana ushindi wa mwisho.

Kwa upande wake Ahmad Jibril ameeleza kufurahishwa kwake na kukutana na Kiongozi Muadhamu na kusema Mapinduzi ya Kiislamu yameifanya Iran kuwa nchi yenye taathira kubwa katika uwanja wa kimataifa na kwamba maendeleo ya sasa ya Iran yamepatikana chini ya usimamizi wa busara na hekima wa Walii wa Waislamu duniani Ayatullah Ali Khamenei. Ahmad Jibril pia amepongeza misimamo imara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kutetea haki za taifa la Palestina.

2767844

captcha