IQNA

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Mapambano dhidi ya mabeberu hayawezi kusimama

15:24 - July 12, 2015
Habari ID: 3327198
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kupambana na mabeberu na mfumo wa kibeberu na kiistikbari kuna misingi katika Qur'ani tukufu na hakuwezi kusimamishwa, na Marekani ndiyo kielelezo kamili cha beberu katika zama hizi.

Ayatullah Khamenei aliyasema hayo Jumamosi jioni mjini Tehran katika hadhara ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kuongeza kuwa kutoka maeneo mbali mbali ya Iran na kuongeza kuwa, Wamarekani na tawala zinazorejea nyuma za Mashariki ya Kati zinaumizwa mno na ushawishi mkubwa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo hili lakini hawawezi kufua dafu. Amesema kuwa idadi kubwa ya vijana wanaojiua barani Ulaya na wimbi la vijana wa Ulaya la kujiunga na kundi la kigaidi la Daesh kwa ajili ya kwenda kujiua kupitia operesheni za kujilipua kwa mabomu ni dalili ya msongo na matatizo ya kinafsi ya tabaka hilo katika nchi za Magharibi. Amewasifu vijana wa Kiirani ambao amesema wameonesha utanashati kwa kushiriki kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds Ijumaa iliyopita baada ya kuhuisha usiku wa Lailatul Qadr kwa ibada na asubuhi yake wakashiriki katika maandamano hayo katika joto kali.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa sababu kuu ya uadui wa madola ya kibeberu dhidi ya taifa la Iran ni kutokubali kwake mfumo wa kibeberu.
Vilevile ameashiria mashambulizi ya siku mia moja na mauaji ya kinyama yanayofanywa na utawala wa Saudi Arabia dhidi ya watu wasio na hatia yoyote wa Yemen na kusema: Nchi za kiliberali za Magharibi zinazodai kutetea uhuru zimenyamaza kimya mbele ya jinai zinazofanywa na Saudia, na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa moja ya maazimio yake ya kuaibisha zaidi kwa kuwalaani watu wanaoshambuliwa wa Yemen badala ya kumlaani mshambuliaji.../mh

3326800

captcha