IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Wananchi, viongozi Iran wawe macho kuhusu njama za maadui

11:35 - August 27, 2015
Habari ID: 3353086
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza juu ya udarura wa wananchi na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa macho mbele ya njama za maadui.

Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo kwa mnasaba wa "Wiki wa Serikali" alipokutana na Rais Hassan Rouhani na baraza la mawaziri ambapo ameyataja kuwa muhimu mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1 katika kutatua mambo na matatizo yake. Vilevile amesisitiza juu ya udharura wa kuwa macho mkabala na mipango ya adui ya kutaka kupenya na kuingia Iran. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, uwezekano wa kutotiliwa maanani malengo ya maadui katika suala la nyuklia ni miongoni mwa wasiwasi na daghadagha zake na kusisitiza kwamba,  tangu mwanzoni mwa Mapinduzi ya Kiislamu hadi leo, uadui wa Wazayuni na Wamarekani dhidi ya Mapinduzi na Jamhuri ya Kiislamu haujapungua na huu ni uhakika ambao kuwepo daima katika fikra za viongozi. Sambamba na Ayatullah Khamenei kusisitiza juu ya kulindwa kasi ya ustawi wa elimu nchini Iran ametilia mkazo suala la kuweko usimamiaji katika uga wa kiutamaduni kwa mujibu wa misingi na nara za Imam Khomeini na Mapinduzi ya Kiislamu. Aidha Kiongozi Muadhamu ameitaja falsafa ya siku za kumbukumbu ya mashahidi Rajai na Bahonar kupewa jina la “Wiki ya Serikali” kwamba, ni kubakisha hai vigezo vya kifikra, kimwenendo na shakhsia ya mashahidi hao wawili azizi. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesifu na kupongeza juhudi za serikali zikiwemo za kufanya hima ya kupunguza ughali wa maisha, kuleta utulivu na uthabiti wa kiuchumi, uzima, afya na kuhitimishwa mazungumzo ya nyuklia.../mh

3352827

captcha