IQNA

Iran kuandaa mashindano ya Qur'ani ya walemavu wa macho

14:46 - January 13, 2016
Habari ID: 3470038
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepanga kuandaa mashindano ya kwanza ya kimataifa maalumu kwa watu wenye ulemavu wa macho.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Dawoud Talfallah, mkuu wa kamatu ya kuandaa mashindano ya Qur'ani Iran amesema mashindano hayo yataandaliwa pambizoni mwa Mashindano ya Kimataifa ya 33 ya Qur'ani Tukufu ya Iran baadaye mwaka huu.

Mashindano hayo hufanyika kila mwaka kwa kuwashirikisha wasomaji na waliohifadhi Qur'ani kutoka maeneo yote ya dunia.

Takfallah amesema nchi baina ya 30-40 zimetangaza kuwa tayari kutuma washiriki katika mashindano hayo ya wale wenye ulemavu wa macho.

Amesema duru hii ya kwanza ya mashindano hayo itajumuisha kuhifadhi Qur'ani tu na kwamba kategoria zingine zitanogezwa katika miaka ijayo.

3466933

captcha